Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amal Jazz Band, bendi ya muziki inayoeneza amani Malakal, Sudan Kusini. 

Watu walioathiriwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini wakiwa katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda raia mjini Malakal
IOM/Bannon
Watu walioathiriwa na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan Kusini wakiwa katika kambi ya Umoja wa Mataifa ya kulinda raia mjini Malakal

Amal Jazz Band, bendi ya muziki inayoeneza amani Malakal, Sudan Kusini. 

Amani na Usalama

Mpango wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS, wanashirikiana na washirika wake wa amani, watu wa Sudan Kusini, kuleta sauti zinazotetea amani ya kudumu katika nchi mpya zaidi ulimwenguni lakini inayoendelea kuteseka na migogoro, vifo na kutawanywa, miaka kadhaa tangu vita ya wenyewe kwa wenyewe.

Ni watoto wa Sudan Kusini wakiwa wameshikilia gitaa kila mmoja, wamekalia viti vya kamba, kila mmoja amevaa barakoa wanafuata kwa umakini maelekezo ya mwalimu wao wa muziki. 

Wanaotoa mafunzo ni wanachama wa kundi la muziki liitwalo Amal Jazz Band kutoka Malakal Sudan Kusini ambayo liliundwa mwaka 2016 na linatumia muziki kuhamasisha amani na umoja miongoni mwa jamii.   

Kwa watoto wengi waliotawanywa, kukulia katika kambi za ulinzi wa raia za Umoja wa Mataifa, masomo ya muziki yanayotolewa na wanachama wa bendi hii, yanaonesha matumaini. Neno Amal, kwa lugha ya kiarabu linaashiria tumaini na ndio maana bendi inatumia jina hili. Fawil John Achuil ni mwanamuziki na mwanachama wa Amal Jazz Band anasema,“kama bendi ya Jazz, tumepiga muziki katika maeneo mengi kote Malakal na kushirkiana na wasanii wengine pamoja na wadau wa misaada ya kibinadamu wa Umoja wa Mataifa kushiriki katika ujenzi wa amani miongoni mwa jamii. Lengo letu ni kupanua ushiriki wa umma katika shughuli za kitamaduni, kuhamasisha muingiliano wa kijamii na kuishi kwa amani miongoni mwa jamii zote Malakal.” 

Kufanya kazi kwa kushirikiana kuleta amani miongoni mwa jamii zote, iwe kwa waliotawanywa au vinginevyo, hivyo ndivyo Amal Jazz Band imejumuisha katika ilani yake pia. Dhamiri hii ya kijamii inaunda uti wa mgongo wa washiriki wote wa bendi kama anavyosisitiza John Achuil, “lengo letu la kwanza la mwisho ni ubinadamu. Hatutaacha kujenga amani na tutaendelea na juhudi zetu kuwakilisha watu wote wa Sudan. Bendi ya muziki ya Amal itadumu kama ishara ya umoja na ubinadamu kama tulivyotangaza katika katiba yetu, katika mipango na maonesho yetu ili tuwakilishe jamii zote. "

Bendi hii ya aina yake inatoa wito kwa wasudan kusini kukumbatia maisha ya kuishi pamoja kwa amani.