Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chuja:

Mashariki ya Kati

Katika muda wa wiki mbili tu, Wapalestina wengi huko Gaza wamepoteza kila kitu nyumba zao, wanafamilia na hali yoyote ya kawaida, wakiwa wamebanwa kwenye vibanda vya kujihifadhi, vyenye chakula na maji kidogo na hakuna umeme, hawajui nini kitatokea siku …
UNDP PAPP/Abed Zagout

Simulizi kutoka Gaza: “Ninatafuta mtandao ili kuangalia maeneo yaliyoathirika huku nikitumai sitaona jina la mume wangu wala familia yangu kwenye orodha”

Hebu vuta tasirwa, mama akiwabembeleza watoto wake usiku, hofu ya kutengana nao ikija kama kivuli, kujaribu awezavyo kujilinda yeye na familia yake, ili ‘wasiwe kumbukumbu’ hata hivyo, hadithi yetu ni kumbukumbu tu sasa, lakini wakati ujao bado haujaandikwa, nikiamka kesho, nataka hili limalizike, ilinirejee mahali patakatifu, kwenye nyumba yetu. 

UN Photo/Evan Schneider
Wajumbe wa Umoja wa Mataifa katika Baraza Kuu wakipigia kura azimio la Gaza katika kikao cha 10 ha dharura.

Baraza Kuu lapitisha rasimu ya azimio la Gaza kulinda raia likitaka usitishwaji mapigano haraka

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa llimepiga kura kupitisha azimio la kulinda raia kwenye mzozo unaoendelea baina ya Israel na Palestina huku katika kikao cha 10 cha dharura ambacho kimefanyika leo kwa siku ya pili kuhu kukiwa na mvutano kwenye Baraza la Usalama na hali katika eneo linalozingirwa la Gaza ikizidi kuwa mbaya.

Mashambulizi ya anga dhidi ya Gaza yanaendelea.
© WHO/Ahmed Zakot

Chonde chonde pande husika sitisheni huhasama, janga kubwa zaidi la kibinadamu laja Gaza: UN

Hali Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amezisihi pande zote katika mzozo kusitisha uhasama , huku mashirika ya misaada yakionya kuhusu janga kubwa zaidi la kibinadamu, wakati hapa Makao Makuu kikao cha 10 cha dharura kuhusu mzozo huo wa Mashariki ya Kati kikiendelea leo. 

 

Sauti
2'53"