Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

HABARI KWA UFUPI:GAZA/UN/ARMENIA

Maji ya kunywa yakigawiwa kwa wakazi na wakimbizi wa ndani Rafah Kusini mwa Ukanda wa Gaza
© UNICEF/Eyad El Baba
Maji ya kunywa yakigawiwa kwa wakazi na wakimbizi wa ndani Rafah Kusini mwa Ukanda wa Gaza

HABARI KWA UFUPI:GAZA/UN/ARMENIA

Msaada wa Kibinadamu

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yataka misaada zaidi ikiwemo mafuta kuingia Gaza, Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa na Theluthi mbili ya watoto wakimbizi waandikishwa shule Armenia

Leo ni siku ya 17 ya kuendelea mzozo wa karibuni baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas huko Mashariki ya Kati ambapo Masharikika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na kilio cha kuongeza misaada zaidi kuingia Gaza kwani iliyowasili hadi sasa haikidhi mahitaji. Shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO likisema limeshindwa kugawa vifaa muhimu vya kuokoa Maisha katika hospitali za Kaskazini mwa Gaza kwa sababu ya kuendelea kwa mashambulizi na kusabbabisha madaktari kufanya upasuaji bila hata ganzi, huku lile na msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA likisema mafuta yamekuwa bidhaa adimu sana na bila mafuta hayo malori ya misaada hayawezi kusafiri na genereta haziwezi kuwasha umeme kwenye hospitali, maduka ya kuoka mikate na kusukuma pampu za maji

Utiaji saini wa Katiba au Chata ya UN tarehe 26 mwezi Juni mwaka 1945  kwenye jengo la maveterani huko San Fransisco, Marekani.
UN Photo/Yould
Utiaji saini wa Katiba au Chata ya UN tarehe 26 mwezi Juni mwaka 1945 kwenye jengo la maveterani huko San Fransisco, Marekani.

Leo ni siku ya UN

Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kumbukumbu ya kuanza kutumika kwa chata iliyoanzisha Umoja huo mwaka 1945. Katika ujumbe wake wa siku hii Clementine Nkweta-Salami naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na kaimu mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu amesema “Mwaka huu tunaadhimisha siku hii wakati Sudan ikikabiliwa na moja ya mgogoro  wa kibinadamu unaokuwa kwa kasi ukiambatana na mahitaji makubwa. Mapigano yamegeuza mgogoro huo kuwa janga kubwa. Zaidi ya watu milioni 5.6 wamefurushwa makwao, milioni 25 wanahitaji msaada, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 4.2 wako katika hatari ya ukajtili wa kijinsia na mtoto 1 kati ya 3 hana fursa ya kwenda shule.

Mwakilishi wa UNICEF Armenia Christine Weigand (Kuhoto) akizuru kituo cha watoto cha UNICEF Goris
© UNICEF/Amar
Mwakilishi wa UNICEF Armenia Christine Weigand (Kuhoto) akizuru kituo cha watoto cha UNICEF Goris

Watoto wakimbizi waandikishwa shule Armenia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema theluthi mbili ya watoto wakimbizi nchini Armenia wameandikiswa katika mifumo ya kitaifa ya shule mwezi mmoja baada ya watoto 21, 000 wenye umri wa kwenda shule kukimbia makwao. UNICEF imesema sasa juhudi ni kuhakikisha watoto walioasalia 1 kati ya 3 ambao hawahudhurii shule wanapata fursa hiyo.