Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza Kuu lapitisha rasimu ya azimio la Gaza kulinda raia likitaka usitishwaji mapigano haraka

Ukumbi wa Baraza Kuu UN wakati wa kikao cha kupiga kura kuhusu azimio kuhusu hali katika Mashariki ya Kati.
Wajumbe wa Umoja wa Mataifa katika Baraza Kuu wakipigia kura azimio la Gaza katika kikao cha 10 ha dharura. UN Photo/Evan Schneider

Baraza Kuu lapitisha rasimu ya azimio la Gaza kulinda raia likitaka usitishwaji mapigano haraka

Amani na Usalama

Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa llimepiga kura kupitisha azimio la kulinda raia kwenye mzozo unaoendelea baina ya Israel na Palestina huku katika kikao cha 10 cha dharura ambacho kimefanyika leo kwa siku ya pili kuhu kukiwa na mvutano kwenye Baraza la Usalama na hali katika eneo linalozingirwa la Gaza ikizidi kuwa mbaya.

Azimio hilo linataka "Suluhisho ya haraka, ya kudumu na endelevu ya kibinadamu baina ya vikosi vya Israel na wapiganaji wa Hamas huko Gaza. Pia linadai utoaji endelevu , kutosha na usiozuiliwa wa vifaa na huduma za kuokoa maisha kwa raia waliokwama ndani ya eneo hilo  na pande zote kuzingatia sheria za kimataifa."

Duru za habari zinaonyesha kuwa Israel imepanua operesheni za ardhini na kuzidisha kampeni yake ya kulipua mabomu.

Mtaa huko Gaza umejaa vifusi vya jengo lililoanguka, huku miundo iliyoharibika ikionekana pande zote mbili.
© UNRWA/Mohammed Hinnawi Mashambulizi ya anga yameharibu sehemu kubwa ya kaskazini mwa Gaza.
Tweet URL

Azimio limepitishwa

Azimio la Jordan limepitishwa na Baraza Kuu, kwa kura 120 za ndio, 14 za kupinga na 45 walijuzuia kupiga kura.

Marekebisho ya rasimu ya azimio yaliyowasilishwa na Canada yameshindwa kupata uungwaji mkono wa kutosha kwani yamepata Kura 85 za kuunga mkono,  55 za kupinga, na 23 hazikupigwa , kwa hivyo rasimu ya azimio la marekebisho hayo halikupita kwa kuwa haikuweza kupata theluthi mbili ya kura zinazohitajika.

Rasimu ya azimio

Rasimu ya azimio linaloongozwa na Jordan kuhusu mgogoro huo inatarajiwa kupigiwa kura mwishoni mwa kikao hicho. 

Rasimu hiyo inaungwa mkono na zaidi ya nchi 40 wanachama, zikiwemo Misri, Oman na Umoja w anchi za Falme za Kiarabu UAE.

Masuala muhimu katika rasimu hiyo ni pamoja na wito wa "makubaliano ya haraka, ya kudumu na endelevu ya kibinadamu pamoja na matakwa kwamba pande zote zifuate sheria za kimataifa za kibinadamu na utoaji wa kuendelea, wa kutosha na usiozuiliwa wa vifaa na huduma muhimu katika Ukanda wa Gaza.

"Pia inatoa wito wa kubatilishwa kwa amri ya Israel, Mamlaka inayokalia kwa mabavu, kwa raia wa Palestina na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa, pamoja na masuala ya kibinadamu na wahudumu wa afya wa kuhamisha maeneo yote katika Ukanda wa Gaza kaskazini mwa Wadi ya Gaza kwa kufuata sheria za kimataifa.”

Marekebisho yamependekezwa na Canada ambayo "inakataa na kulaani mashambulizi ya kigaidi ya Hamas nchini Israel kuanzia tarehe 7 Oktoba na kuchukuliwa kwa mateka.”

Rasimu ya maazimio hayawakilishi msimamo rasmi wa Baraza Kuu hadi yatakapopitishwa.

 

Israeli: Siku ya Ushindi usiokubalika

Balozi Gilad Erdan wa Israel akizungumza katika mkutano wa Baraza la Usalama UN mjini New York.
United Nations Balozi Gilad Erdan wa Israel akizungumza baada ya azimio la Gaza kupitishwa wakati wa kikao cha 10 cha dharura cha Baraza Kuu kuhusu hali ya eneo linalokaliwa la Palestina

 Balozi wa Israel kwenye Umoja wa Mataifa, akitoa kauli baada ya kupitishwa azimio hilo amesema "Leo ni siku ambayo itaingia katika historia mbayá. Sote tumeshuhudia kwamba Umoja wa Mataifa hauna hata chembe moja ya uhalali. Umoja wa Mataifa umejitolea kuhakikisha ukatili zaidi. Kwa mujibu wa familia ya mataifa, Israeli haina haki ya kujilinda.”

Ameendelea kusema kwamba hakuna mazungumzo au majadiliano yatakayofanyika na Hamas, na kuwa Israel haitakaa kimya kuwaacha wafanye ukatili tena. Azimio hilo haliitaji Hamas hata mara moja, kana kwamba vita vilianza peke yake.

“Ni nini kinaendelea hapa?” aliuliza, akihoji endapo lengo lilikuwa kufunga mikono ya Israeli. Amesema “Njia pekee ya kuangamiza Hamas ni kuwang’oa. Kwa nini hamuwawajibishi Hamas?”

Balozi Erdan amesema "Tunajua hakuna mgogoro wa kibinadamu kwa mujibu wa sheria ya kimataifa ya kibinadamu," akibainisha kuwa kila takwimu inatoka Hamas ya habari kuhusu Gaza.

Hakuishia hapo ameongeza kuwa yeyote anayetaka kuzuia ghasia anapaswa kutoa wito kwa Hamas kuweka chini silaha zao, kujisalimisha na kuwarudisha mateka wote.

"Ikiwa hili lingetokea, vita vitaisha mara moja," amesema. "Hii ni siku ya giza kwa Umoja wa Mataifa na wanadamu. Israel itajilinda na itafanya kile ambacho ni lazima kifanyike ili kuangamiza uwezo wa Hamas na kuwarudisha mateka nyumbani.”

Nchi zingine mbalimbali zilizungumza kabla ya upigaji kura huo uliofanyika kwa awamu mbili.

Balozi Munir Akram wa Pakistan akizungumza katika mkutano wa UMOJA WA MATAIFA.
United Nations Balozi Munir Akram wa Pakistan akizungumza kabla ya upigaji kura kwenye Baraza Kuu katika kikao cha 10 cha dharura

Pakistan: Israeli lazima itajwe pia

Katika hotuba yenye nguvu inayopinga maelezo ya Canada, balozi wa Pakistan Munir Akram alisema kwamba kama Canada ingefanya haki katika marekebisho yake ingekubali kuitaja Israel na Hamas.

Kutotaja upande wowote lilikuwa chaguo bora zaidi amesema, kama azimio la Jordan linavyofanya.

"Israeli inahitaji kutajwa pia, ikiwa unataka kuwa wa haki na usawa ", alisema.

Sote tunajua ni nani aliyeanzisha hii vita. Ni miaka 50 ya uvamizi wa Israel na mauaji ya Wapalestina bila ya kuadhibiwa, aliongeza.

Israeli haiwezi kukabiliana na ukweli au kukabiliana na haki. Ukaliaji wa Israel ni dhambi ya asili, sio kile kilichotokea tarehe 7 Oktoba.

Upigaji kura kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa

Katika Baraza Kuu nchi wanachama 193 kila moja ina kura moja, na tofauti na Baraza la Usalama, hakuna kura ya turufu.

Maamuzi ya Baraza Kuu kuhusu masuala muhimu hufanywa na theluthi mbili ya wajumbe waliopo na kupiga kura. 

Masuala haya ni pamoja na: mapendekezo kuhusu udumishaji wa amani na usalama wa kimataifa, au masuala mengine yaliyofafanuliwa chini ya kanuni ya 83 ya kanuni za taratibu za Baraza Kuu.

Maamuzi kuhusu masuala mengine isipokuwa yale yaliyotolewa katika kanuni ya 83, ikijumuisha uamuzi wa vipengele vya ziada vya masuala yatakayoamuliwa na theluthi-mbili ya walio wengi, hufanywa na wajumbe wengi waliopo na kupiga kura.

Maneno "wanachama waliopo na wanaopiga kura" inamaanisha wanachama wanaopiga kura ya ndio au hapana.

Wanachama ambao hujiepusha na kupiga kura wanachukuliwa kuwa hawakupiga kura.

Waangalizi wa kudumu wa Umoja wa Mataifa, Holy See na Palestina hawana kauli katika maamuzi ya Baraza Kuu.