Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Taarifa kuhusu Virusi vya Corona

Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

27 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Watoto wengi wakosa chanjo hata kabla ya  kuzunga kwa janga la virusi vya Corona au COVID-19 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likitaka hatua madhubuti zichukuliwe sasa kuhakikia watoto wanapata chanjo zote

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo limeanza kusambaza mashine za hewa ya Oxygen katika vituo sita vya afya vinavyohudumia wagonjwa wa COVID-19

Sauti
11'
© UNICEF/Frank Dejongh

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Suala la unyanyapaa wa aina yoyote ile ni mtihani mkubwa katika jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao hutoa wito kila uchao kuhakikisha changamoto hiyo inatokomezwa .Wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 unyanyapaa umeelezwa kujitokeza na kusababisha changamoto kwa wagonjwa na washukiwa na hata kuwafanya wengine kutojitokeza kufanya vipimo hali ambayo shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kuwa ni hatari kubwa na kikwazo cha kupambana na ugonjwa huo.

Sauti
6'25"

24 APRILI 2020

Katika Jarida la Habari hii leo Flora Nducha anakuletea

-Mwezi mtukufu wa Ramadhani unaanza leo kote duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa awatakia kila la heri Waislam wote na kusema kwamba COVID-19 itaifanya Ramadhan ya mwaka huu kuwa tofauti kabisa

-Kamishina Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa Michelle Bachelet amesema anatiwa hofu na kamatakamata na kubanwa kwa vyombo vya habari wakati huu wa janga la COVID-19 ambapo taarifa sahihi ni muhimu sana

Sauti
10'46"

23 APRILI 2020

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

Umoja wa Mataifa wasema teknolojia ya mawasiliano imedhihirisha umuhimu wake hasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 na hivyo kuhimiza wasichana wengi wawezeshwe kuingia katika teknolojia hiyo ya ICT

-Vifaa na misaada kutoka kituo kikuu kilichopo Addis Ababa Ethiopia vyaleta mabadiliko kwa maelfu ya watu katika vita dhidi ya COVID-19 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP

Sauti
11'13"