Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 APRILI 2020

27 APRILI 2020

Pakua

Katika Jarida la Habari la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

-Watoto wengi wakosa chanjo hata kabla ya  kuzunga kwa janga la virusi vya Corona au COVID-19 limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF likitaka hatua madhubuti zichukuliwe sasa kuhakikia watoto wanapata chanjo zote

-Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC , shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF leo limeanza kusambaza mashine za hewa ya Oxygen katika vituo sita vya afya vinavyohudumia wagonjwa wa COVID-19

- Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo IFAD  ukishirikiana na wadau wamepusha mizozano kati ya wakimbizi na wafugaji  nchini Niger kwa kuanzisha mradi wa maji ambayo ni bidhaa adimu katika jamii hizo

-Makala leo inatupeleka Pangani mkoani Tanga nchini Tanzania utamsikia afisa wa serikali akielezea hatua wanaochukua kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi

-Na mashinani tuko Ngorongoro Tanzania afisa hifadhi katika mbuga hiyo anafafanua jinsi teknolojia inavyowawesesha watalii kuendelea kufurahia wanyama wa mbuga hiyo

Audio Credit
UN News/Flora Nducha
Audio Duration
11'