23 APRILI 2020

23 Aprili 2020

Katika jarida la Umoja wa Mataifa hii leo Flora Nducha anakuletea 

Umoja wa Mataifa wasema teknolojia ya mawasiliano imedhihirisha umuhimu wake hasa wakati huu wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 na hivyo kuhimiza wasichana wengi wawezeshwe kuingia katika teknolojia hiyo ya ICT

-Vifaa na misaada kutoka kituo kikuu kilichopo Addis Ababa Ethiopia vyaleta mabadiliko kwa maelfu ya watu katika vita dhidi ya COVID-19 limesema leo shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula WFP

-Shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO  limesema mipango ya dharura  ni lazima iwekwe ili chanjo ziendelee wakati huu wa janga la COVID-19 kuweza kunusuru maisha ya mamilioni ya watoto kutokana na magonjwa yanayoweza kuzuilika kwa chanjo

-Makala leo inaturejesha Uganda katika sehemu ya pili ya simulizi ya biti aliyepata mimba ya utotoni leo anaeleza matumaini yake ya maisha yalivyorejea baada ya kujifungua

-Na mashinani tuko Zimbabwe  kwa Precious Khumalo, Afisa Mkuu wa Programu ya Musasa inayohusika na masuala ya kuokoa maisha ya manusura wa ukatili wa kijinsia

-

Audio Credit:
UN News/Flora Nducha
Audio Duration:
11'13"

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud