Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Unyanyapaa ni changamoto kubwa katika vita dhidi ya COVID-19 Uganda

Pakua

Suala la unyanyapaa wa aina yoyote ile ni mtihani mkubwa katika jamii kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ambao hutoa wito kila uchao kuhakikisha changamoto hiyo inatokomezwa .Wakati huu wa mlipuko wa janga la virusi vya Corona au COVID-19 unyanyapaa umeelezwa kujitokeza na kusababisha changamoto kwa wagonjwa na washukiwa na hata kuwafanya wengine kutojitokeza kufanya vipimo hali ambayo shirika la afya ulimwenguni WHO limeonya kuwa ni hatari kubwa na kikwazo cha kupambana na ugonjwa huo. nchini Uganda, mwandishi wetu John Kibego amefuatilia hali ilivyo ya unyanyapaa na jinsi unavyozorotesha juhudi za kudhibiti virusi hivyo mji wa Hoima alipotembelea baadhi ya familia za waliokamilisha siku   za karantini.

Audio Credit
UN News/John Kibego
Audio Duration
6'25"
Photo Credit
© UNICEF/Frank Dejongh