Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nchini Uganda na Afrika Kusini, UN yazindua ombi la ufadhili kupambana na COVID-19 

Masoko yafungwa nchini Uganda wakati serikali ikichukua hatua kukabiliana na kusambaa kwa COVID-19.
UN News/ John Kibego
Masoko yafungwa nchini Uganda wakati serikali ikichukua hatua kukabiliana na kusambaa kwa COVID-19.

Nchini Uganda na Afrika Kusini, UN yazindua ombi la ufadhili kupambana na COVID-19 

Afya

Nchini Uganda, ambako kuna wagonjwa 56 wa COVID-19, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo, Rosa Malango hii leo amezindua ombi la dharura la dola milioni 316 za Marekani kwa ajili ya kushughulikia janga hili. 

Fedha zinazoombwa zinalenga kushughulikia maeneo matano muhimu ambayo ni afya, uhakika wa chakula, ustawi wa maisha na lishe, huduma za kuokoa maisha pamoja na ulinzi wa jamii, wakimbizi na kuwahamisha watu pamoja na msaada wa  haraka wa kuimarisha uchumi ikiwemo uvumbuzi wa kidijitali.

Timu ya Umoja wa Mataifa pia inaelekeza takribani dola milioni 13.5 kutoka katika ufadhili wao wa kawaida kwa ajili yakushughulikia ugonjwa wa COVID-19

Kwa kushirikiana kwa ukaribu na serikali kwa ngazi ya kitaifa na ngazi za chini, mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini Uganda yatatimiza majukumu kwa kushirikiana pia na mashirika yasiyo ya kiserikali pamoja na shirika la msalaba mwekundu la Uganda.

Zaidi ya COVID-19, Uganda pia inakabiliwa na milipuko ya magonjwa kama homa ya manjano katika eneo la Nile Magharibi, na surua katika wilaya 13. Pia homa ya Crimean Congo Hemorrhagic.

Bi Malango ameonya kwamba hatari za janga la virusi vya corona inaweza kuwa kuathirika kwa uchumi wa Afrika Mashariki hususani kwa watu waliko katika mazingira hatarishi kama asilimia 85 ya wanawake na asilimia 91 ya vijana kwenye sekta isiyo rasmi. Pia kaya zinazoongozwa na watoto, wakimbizi, wazee, watu wenye ulemavu, wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI na kifua kikuu pamoja na watu walio maskini mijini na vijijini. inayoathiri moja ya uchumi muhimu zaidi wa Afrika Mashariki na athari inayowezekana kwa watu walio katika mazingira hatarishi, kama asilimia 85 ya wanawake na asilimia 91 ya vijana kwenye sekta isiyo rasmi, kaya zinazoongozwa na watoto, wakimbizi, wazee, walemavu, watu wanaoishi na VVU au ugonjwa wa kifua kikuu pamoja na masikini katika maeneo ya mijini na vijijini, pamoja na watu waliolazimishwa kuteleza ndani kwa sababu ya hali ya hewa kali. Alitoa wito kwa ulimwengu kuunga mkono juhudi za UN kupata Uganda na nchi zingine kufuata Malengo ya Maendeleo Endelevu ili kuhakikisha kuwa na njaa, upatikanaji wa huduma za kimsingi, pamoja na afya, usafi wa mazingira, elimu na miundombinu ya msingi inayowezesha jamii kufanikiwa.

Kwa upande wa Afrika Kusini, ambako kuna wagonjwa waliothibitika 3500 walio na COVID-19, Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini humo Nardos Bekele-Thomas anaongoza timu ya Umoja wa Mataifa katika kuunga mkono juhudi za serikali za kushughulikia mahitaji ya kiafya na madhara ya kijamii na kiuchumi yanayosababishwa na mlipuko huu wa virusi vya corona. Pande zote zinajiandaa kutoa ombi la ufadhili ili kuongeza nguvu ya mapambano. Kwa upande wake UNHCR wametoa nyongeza ya dola 600, 000, mchango kwa serikali  ikiwa ni nyongeza katika programu iliyopo hivi sasa ya dola milioni 6.8. 

Pia ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na madawa na uhalifuUNODC imechangia vifaa vya kujikinga katika makazi mjini Pretoria na Durban kwa wanawake wanaosaka hifadhi kutoka kwa wenza wao ambao wanawanyanyasa. Shirika la wanawake la Umoja wa Mataifa UN Women, pia inafanya kazi kushughulia madhara ya COVID-19 ikiwasaidia wanawake wakulima katika hatua za kujilinda ikiwa ni pamoja na kupata vibali vya kusafiri ili waendelee kuuza katika masoko. 

Afrika Kusini ikiwa ni moja ya nchi duniani zenye maambuki ya juu ya VVU, shirika la Umoja wa Mataifa la kupambana na UKIMWI, UNAIDS inasambaza dawa kwa watu wanaoishi na VVU/UKIMWI au magonjwa mengine kama Kifua Kikuu ambayo yanawaweka watu katika hatari ya kushambuliwa na COVID-19.