Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu ni tofauti kabisa- Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifanya mkutano kupitia mtandao kuhusu janga la kimataifa la COVID-19
UN Photo/Loey Felipe
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akifanya mkutano kupitia mtandao kuhusu janga la kimataifa la COVID-19

Mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani mwaka huu ni tofauti kabisa- Guterres

Amani na Usalama

Waumini wa dini ya kiislamu ulimwenguni wakianza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake wa kuwatakia heri katika mfungo wa sasa ambao amesema ni tofauti kabisa na mingine iliyotangulia kwa ajili ya janga la COVID-19.

Waumini wa dini ya kiislamu ulimwenguni wakianza kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametoa ujumbe wake wa kuwatakia heri katika mfungo wa sasa ambao amesema ni tofauti kabisa na mingine iliyotangulia.

Bwana Guterres amesema utofauti huo unatokana na janga la ugonjwa wa virusi vya Corona, au COVID-19 ambalo amesema harakati za kupambana nalo  zinaathiri shughuli nyingi za kijamii.

Amesema pamoja na janga hilo, bado watu wengi katika maeneo ya vita, kwa mara nyingine kwa bahati mbaya  watakuwa wanafunga mwezi huu mtukufu na vita na ukosefu wa usalama pande zote.

Katibu Mkuu amekumbusha wito wake wa hivi karibuni wa kutaka kusitishwa mapigano kwa haraka ulimwenguni kote ili kujikita na adui yetu wa pamoja- virusi.

“Narejea wito huo leo nikikumbusha maneno ya Quran tukufu  Na endapo wataisaka amani,   basi nawe ishikilie” Ramadhani pia maana yake ni kusaidia wasiojiweza . Nazishukuru serikali na watu kutoka ulimwengu wote wa kiislam wanaoishi kwa imani yao na kuwasaidia wanaokimbia machafuko, kwa njia bora ya desturi ya kiislam ya wema na ukarimu, somo muhimu katika dunia hii ambako milango mingi imefungwa kwa wale wanaohitaji ulinzi hata kabla ya COVID-19.”

Katibu Mkuu pamoja na kuwatakia waumini wa dini ya kiislamu mfungo mwema, ameomba pia kuwepo kwa mshikamano na huruma katika nyakati hizi za majaribu.