Virusi vya Corona kama dharura ya afya ya umma:Taarifa za UN News Kiswahili
Mlipuko uliripotiwa mara ya kwanza Wuhan China Desemba 31, 2019

Ukurasa huu unaleta pamoja taarifa kuhusu muongozo kutoka kwa Shirika la afya la Umoja wa Mataifa, WHO na Umoja wa Mataifa kuhusu mlipuko wa sasa wa virusi vya corona au COVID-19, ambavyo viliripotiwa mara ya kwanza Wuhan, China mnamo Desemba 31, 2019. Tafadhali tembelea ukurasa huu kupata taarifa za kila siku. WHO inafanya kazi kwa karibu na wataalam wa kimataifa, serikali na wadau kupanua ujuzi wa kisayansi kuhusu virusi hivi vipya, kutokana na jinsi vinavyosambaa na athari zake  na kutoa ushauri kwa nchi na watu, kuhusu hatua za kuchukua kwa ajili ya kulinda afya na kuzuia kuenea kwa mlipuko.

Ujumbe wangu kwa G20 ni rahisi: Tunahitaji mshikamano na ushirikiano-Guteress 

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres akiwahutubia wanahabari hii leo mjini New York Marekani, kuhusu mkutano wa kesho wa viongozi wa nchi 20 zilizo na uchumi mkubwa duniani, G20, ameanza kwa kueleza kuwa mkutano huu unakuja wakati ambao janga la COVID-19 linaendelea kuuharibu ulimwengu. 

Homa ya kichomi huwaacha Watoto milioni 4.2 wakihaha bila oksijeni kila mwaka:Ripoti

Tathimini mpya iliyotolewa leo na mashirika ya kimataifa ukiwemo Umoja wa Mataifa imesema takribani watoto milioni 4.2 wa chini ya umri wa miaka mitano wanaathirika na uhaba wa hewa ya oksjeni kutokana na homa kali ya kichomi au pneumonia.  

COVID-19 yaathiri wahamiaji na utumaji fedha nyumbani 

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini kuwa viwango vya  njaa na ukimbizi ambavyo tayari vilikuwa vimevunja rekodi kabla ya mlipuko wa wa ugonjwa wa Corona au COVID-19,  vitazidi kuongezeka wakati huu ambapo wahamiaji na wategemezi wa fedha kutoka nje wanahaha kusaka kazi ili kusaidia familia zao. 

Njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu dunian-UN

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamezikosoa nchi zinazojaribu kubinafsisha na kuhodhi chanjo yoyote ya dhidi ya corona au COVID-19 inayotarajiwa kupatikana wakisema njia p

Sauti -
2'22"

Hifadhi ya Dja Cameroon yachukua hatua kupambana na COVID-19 

Maeneo mengi ya hifadhi za viumbe hai na misitu pamoja na mbuga za wanyama pori yameathirika kwa namna moja au nyingine kutokana na uwepo wa mlipuko vya virusi vya corona ulimwenguni. Hifadhi ya Dja nchini Cameroon ni miongoni mwa waathirika, lakini ambao wanafanya chini juu kujikinga na kujikwamua na hali hiyo.

Hakuna mtu atakayekuwa salama hadi wote watakapokuwa salama dhidi ya COVID-19:UN 

Wataalam wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo wamezikosoa nchi zinazojaribu kubinafsisha na kuhodhi chanjo yoyote ya dhidi ya corona au COVID-19 inayotarajiwa kupatikana wakisema njia pekee ya kupambana na janga hili ni kuhakikisha chanjo inapatikana kwa gharama nafuu kwa kila mtu duniani.

Kando na madhila yatokanayo na COVID-19 kwa upande mwingine imetoa fursa ya ubunifu

Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la

Sauti -
2'51"

COVID-19 inahimiza ubunifu wa kiafya barani Afrika-WHO

Utafiti mpya wa Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa WHO uliotangazwa katika mji mkuu wa Jamhuri ya Congo, Brazzaville, umesema janga la COVID-19 limeongeza nguvu kwenye maendeleo ya ubunifu zaidi ya 120 wa teknolojia ya afya ambao umejaribiwa au kupitishwa barani Afrika.

Mashahiri yatumika kupinga ukatili kwa watoto miongoni mwa wakimbizi Uganda wakati wa COVID-19  

Kufuatia mlipuko wa COVID-19 mnamo Machi mwaka huu nchini Uganda, shule zilifungwa na hivyo kuwaweka hatarini watoto kukumbana na ukatili wa kijinsia hasa katika makazi ya wakimbizi ambako hud

Sauti -
3'29"

Dunia iko katika janga la tsunami ya COVID-19: Guterres 

Ikiwa leo ni siku ya uelimishaji kuhusu tsunami duniani Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameitaka dunia kuiba uzoefu wa maandalizi ya majanga kwenye hatua zilizopigwa katika kupunguza vifo vitokanavyo na tsunami.