Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Alihesabiwa siku za kuishi lakini akaishi zaidi

Evelyne na mwanae aliyejifungua salama baada ya kuwa na VVU. Picha: UM/Video capture

Alihesabiwa siku za kuishi lakini akaishi zaidi

Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo usambazaji wa huduma za kujikinga na virusi vya ukimwi, VVU ikiwa ni moja ya utekelezaji wa lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs.

Umoja wa Mataifa unaendelea kupigia chepuo usambazaji wa huduma za kujikinga na virusi vya ukimwi, VVU ikiwa ni moja ya utekelezaji wa lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs. Lengo hilo la ustawi wa afya kwa wote linaangazia siyo tu Malaria na Kifua Kikuu bali pia Ukimwi ambao unaendelea kuwa tishio, licha ya kwamba tayari kuna kinga. Huko nchini Kenya, mwanamke mmoja ambaye baada ya kukatiwa tiketi ya kifo, alikata tamaa akaona dunia imemgeuka. Lakini baada ya kuamua kuchukua hatua, nuru ikaingia na hata akaweza kuongeza familia yake. Je alifanya nini ? Ungana basi na Assumpta Massoi kwenye makala hii.