Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ugunduzi wa rasilimali ya mafuta huwa ni wa kujivunia lakini unakuja na changamoto zake

Ugunduzi wa rasilimali ya mafuta huwa ni wa kujivunia lakini unakuja na changamoto zake

Pakua

Ugunduzi wa rasilimali ya mafuta hua ni wa kujivunia kwani huleta fursa nyingi zikwemo ajira, ukwaji wa miji, viwanda na hata uchumi wa taifa kwa ujumla.

Lakini kwa upande mwingine hua na madhara kwa mazingira na jamii ambayo huathiri zaidi watu wa kipato cha chini katika jamii husika.

Uganda inajiandaa kuanza kuzalisha mafuta katika eneo la Bonde la Ufa la Ziwa Albert ambapo sasa wanamazingira wanaonya kuhusu athari za viwanda vya mafuta wakati ambapo misitu ya asili inazidi kuchafuliwa kwa ajili ya kilimo na makaazi.

Je, wanasema ini?

Basi uungana na John Kibego katika makala hii ambapo amezungmuza na Robert Byaruhanga, mtaalamu wa mazingira kufahamu kwa undani uhusiano kati ya misitu, viwanda na mabadiliko ya tabianchi.

(Makala ya John Kibego)

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'50"
Photo Credit
UN News/ John Kibego