Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watu wanafikiri Umoja wa Mataifa ni shirika moja tu-Balozi Manongi

Watu wanafikiri Umoja wa Mataifa ni shirika moja tu-Balozi Manongi

Pakua
Jumapili hii ulimwengu unaadhimisha siku ya Umoja wa Mataifa ambayo mwaka huu inabeba kilele cha maadhimisho ya Umoja huo kutimiza miaka 75 tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1945. Umoja huo umepitia katika mabonde na milima mingi lakini lengo lake kuu la kutunza amani ya ulimwengu na kupafanya mahali bora pa kuishi limeendelea pasina kutetereka. 
 
Balozi Tuvako Manongi, mwanadiplomasia aliyebobea na aliyepata kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa anaeleza faida za Umoja wa Mataifa kwa ulimwengu hususani kwa nchi zinazoendelea. 
Audio Credit
Grace Kaneiya/ Tuvako Manongi
Audio Duration
3'36"
Photo Credit
UN Photo/Rick Bajornas)