Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya changamoto, mwanamke wa kijiji bado anajitahidi kujikwamua

Licha ya changamoto, mwanamke wa kijiji bado anajitahidi kujikwamua

Pakua

Hivi karibuni dunia imeadhimisha siku ya mwanamke wa kijijini ikimulika harakati zao na changamoto wanazokumbana nazo hasa wakati huu wa janga la ugonjwa wa virusi vya Corona au COVID-19. Kundi hili limegubikwa na changamoto kama vile huduma za kijamii na kiuchumi na hivyo janga la COVID-19 kuwa sawa na kuongeza chumvi kwenye kidonda. Ingawa hivyo wanawake hao hawajakata tamaa na wanahaha kuhakikisha kwamba wanasonga mbele huku mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo lile la kuhudumia watoto, UNICEF likipendekeza hatua mujarabu ya malezi kwa watoto ili makuzi yao yaweze kujenga jamii imara vijijini.

Devotha Songorwa wa radio washirka Kids Time FM nchini Tanzania amekutana na baadhi ya wanawake wa kijiini na kuzungumza nao ili kufahamu changamoto wanazopitia na harakati za kujikwamua.

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ Devotha Songorwa
Audio Duration
3'54"
Photo Credit
UN News/Assumpta Massoi