Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vijana waonywa dhidi ya matapele wanaposaka ajira katia sekta ya mafuta, Uganda

Vijana waonywa dhidi ya matapele wanaposaka ajira katia sekta ya mafuta, Uganda

Pakua

Kutokana na kiwango kikubwa cha ukosefu wa ajira miongoni mwa vijana katika nchi nyingi duniani, baadhi ya vijana wamejikuta katika mazingira ya kunyang’anywa kidogo walichonacho kupitia mikono ya matapeli.

Hali si tofauti nchini Uganda mabapo uzalishaji wa mafuta unanyemelea katika Bonde la Ufa la Ziwa Albert.

Taarifa zinasema tayari vijana kadhaa wamekuwa waathirika wa utapeli kwa kulipa pesa kama moja ya masharti ya kupata kazi mbalimbali katika makampuni ya mafuta yaliyoanza upya kufanya kazi baada ya kusitishwa kutokana na mlipuko wa COVID-19.

Je, imekuaje? Ni fursa gani kwa ukweli zilizopo sasa?

Pata maelezo zaidi katika makala ifuatayo  ambapo John Kibego anamhoji afisa wa mawasiliano wa kampuni ya mafuta ya Ufaransa ya Total E&P Uganda kuhusu hali hiyo. 

 

Audio Credit
Grace Kaneiya/ John Kibego
Audio Duration
3'53"
Photo Credit
Picha: UNICEF/Al-Zikri