Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika

'Hatuhamihami" bali tunahama na tutarejea- Dkt. Laltaika

Pakua

Mvutano mkubwa huibuka baina ya wakulima na jamii ya watu wa asili hususan ile ya wafugaji. Mvutano huo ni katika masuala ya matumizi ya ardhi ambapo mara nyingi wafugaji hulaumiwa kutumia ardhi kiholela kutokana na kuhama kwao wanaposaka malisho ya mifugo yao. Umoja wa Mataifa unasisitiza masuala ya matumizi bora ya ardhi kama njia ya kulinda tabianchi Je ni kweli wafugaji  huhamahama? Na je kupitia wafugaji hasa wa jamii ya asili ,dunia inaweza kubadili mweleko wa sasa wa uharibifu wa mazingira na tabianchi. Assumpta Massoi amezungumza na Dkt. Elifuraha Laltaika, mmoja wa wataalamu 16 wa jukwaa la kudumu la Umoja wa Mataifa la watu wa jamii ya asili.  Dkt. Laltaika anaanza kwa  kuelezea ardhi na matumizi yake kwa jamii ya watu wa asili hususan wafugaji.

Audio Credit
Selina Jerobon, Assumpta Massoi
Audio Duration
4'8"
Photo Credit
UN News