Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makabila Kenya sasa ni 44, ni baada ya wamakonde na wahindi nao kutambuliwa

Makabila Kenya sasa ni 44, ni baada ya wamakonde na wahindi nao kutambuliwa

Pakua

Uhamiaji kwa sasa unakumbwa na madhila makubwa. Watu wanahama kwa sababu mbalimbali ikiwemo kusaka maisha bora, elimu, ajira, kuanzisha familia na nyingine nyingi. Nchini Kenya wahamiaji walitoka mbali hata bara hindi na nchi jirani kama vile Tanzania na Msumbiji. Kenya imechukua hatua kuunga mkono utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu, SDGs hususan lengo namba 10 la kutaka mienendo salama ya binadamu ikiwemo uhamiaji bora. Sasa wageni wanapata uraia nchini Kenya na kunufaika na huduma mbalimbali. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa idhaa hii amezungumza na Nzomo Mulatya ambaye ni Naibu Mkurugenzi wa Baraza la Kitaifa la idadi ya watu nchini Kenya na Bwana Mulatya anaanza kwa kuzungumzia idadi ya makabila waliyoongeza.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
4'2"
Photo Credit
UN News/Selina Jerobon