Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Winnie Mandela-shujaa aliyebeba mkuki kutetea wanyonge

Winnie Mandela-shujaa aliyebeba mkuki kutetea wanyonge

Pakua

Winnie Nomzamo  Madikizela Mandela! aliaga dunia mwezi huu wa Aprili! Daima atakumbukwa kwa harakati zake za ukombozi wa taifa la Afrika Kusini dhidi ya  ukatili wa ubaguzi wa rangi ulioshamiri nchini humo karne ya 20. Ma Winnie kama alivyojulikana zaidi licha ya taswira yake kukumbwa na misukosuko wakati wa uhai wake, kifo chake kiligeuka fursa kwa watu wengi kuweza kumfahamu zaidi na kujifunza tofauti na mengi maovu yaliyosemwa wakati wa uhai wake.

Umoja  wa Mataifa kwa kutambua harakati za Mama Winnie za za kutetea  haki za binadamu, ulifanya tukio maalum jijini NEw York, Marekani! Assumpta Massoi ameandaa makala inayoangazia tukio hilo.

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
3'58"
Photo Credit
UN Photo/Eskinder Debebe)