Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

10 NOVEMBA 2023

Ungana na Leah Mushi kusikia haya jaridani hii leo:

Hofu ya uhalifu wa vita ikitanda UN yataka jinamizi linaloghubika Gaza liishe.

UNMISS yawajengea wanajeshi wa Sudan Kusini uwezo kulinda haki za watoto.

UNCDF na EU katika harakati za kuwakwamua wananchi Gambia dhidi ya mabadiliko ya tabianchi.

Na mashinani msichana ambaye ni mkimbizi wa ndani nchini Sudan.

Sauti
13'7"

09 NOVEMBA 2023

Hii leo Jaridani Evarist Mapesa anakuletea mada kwa akina inayoangazia kazi za majumbani na utasikia kisa cha mtoto wa miaka 11 kutoka nchini Tanzania ambaye akiwa na miaka 10 alikuwa akitumikishwa pamoja na madhila mengine aliyokumbana nayo. 

Pia utasikia habari kwa ufupi zikiangazia masuala ya kibinadamu kwa wananchi wa Gaza na masuala ya mazingira. 

Na leo katika kujifunza Kiswahili utasikia ufafananuzi wa methali Umekuwa bata akili kwa watoto. 

Msomaji wako ni Leah Mushi.

Sauti
11'36"

08 NOVEMBA 2023

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mwelekeo wa El Nino ya kwamba itaendelea hadi Aprili 2024,  halikadhalika madhara  yake, Somalia kulekea uchaguzi mkuu na ushiriki wa wanawake; Makala inabisha hodi Mashariki ya Kati usaidizi wa kibinadamu huko Gaza, na mashinani inabisha hodi Armenia.

Sauti
9'49"

07 Novemba 2023

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Umoja wa Mataifa ulikuwa na siku tano za kuadhimisha Umoja wa Mataifa kutimiza miaka 78 tangu kuanzishwa kwake mwaka 1945 huko San Fransisco nchini Marekani.  Maadhimisho yalifanyika kuanzia tarehe 23 hadi 27 Oktoba kwenye mji mkuu, Kinshasa. Byobe Malenga, mwandishi wetu katika taifa hilo la Maziwa Makuu ndio alikuwa shuhuda wetu wa nini kilifanyika.

Sauti
11'45"

06 NOVEMBA 2023

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia Mashariki ya Kati, mapigano huko Gaza siku ya 30, "imetosha" yasema mashirika ya kimataifa, kisha anakwenda Gambia, Magharibi mwa Afrika huko kalavati limeimarisha afya. Makala ni kijana Emmanuel Cosmas Msoka akizungumza na Flora Nducha kuhusu SDGs na mashinani tunakwenda Karamoja nchini Uganda, kilimo cha kisasa kimekomboa wanawake kiuchumi na kijamii. 

Sauti
12'59"

03 NOVEMBA 2023

Karibu kusikiliza jarida la Umoja wa Mataifa ambapo hii leo utasikia kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu OHCHR ambayo imesikitishwa sana na ripoti kwamba huko Darfur nchini Sudan wanawake na wasichana wanatekwa nyara na kushikiliwa katika mazingira ya yasiyo ya kiutu katika maeneo yanayodhibitiwa na wanamgambo waasi (RSF). 

Pia utapata ufafanuzi wa Ibara ya 12 ya Tamko la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu ambalo mwaka huu linatimiza miaka 75. 

Sauti
10'