Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

14 NOVEMBA 2023

14 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo licha ya mashambulizi dhidi ya vituo vya afya na makazi ya watu katika Ukanda wa Gaza, mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yanaendelea kujitahidi usiku na mchana kuhakikisha watu wanapata huduma ya afya ili kuokoa maisha yao lakini ni wazi kwamba hali inazidi kuwa mbaya kila uchao. Pia tunakuletea habari kwa ufupi na mashinani.   

  1. Huko Gaza Mashariki ya Kati madhila kwa raia yanaendelea na leo shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO limepongeza ujasiri wa juhudi za wahudumu wa afya katika hospitali ya Al-shifa  na kuelezea hofu yake kwa maelfu ya watu waliotawanywa na mgogoro unaoendelea kufuatia mvua kubwa zinazonyesha ambazo zimesababisha mafuriko na kufanya hali ya ya kibinadamu iliyokuwa mbaya kuwa mbaya zaidi. Nalo Shirika la Umoja wa Mataifa la msaada kwa wakimbizi wa Kipalestina UNRWA limeonya kuhusu ukosefu wa mafuta likisema sasa akiba yote imekwisha, malori yake hayawezi kufanya kazi na hivyo hayataweza kupokea msaada kutoka kivuko cha Rafah, nusu ya hospital zote Gaza hazifanyikazi kwa kukosa mafuta na 14 zinazoendelea kufanyakazi hazina mafuta ya kutosha na vifaa muhimu vinavyohitajika huku mawasiliano yakiendelea kuwa changamoto kubwa. 
  2. Tukiendelea na madhila kwingineko nchini Sudan shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema leo kwamba mlipuko mpya wa kipindupindu unaongeza shinikizo katika hali mbaya ya kibinadamu nchini humo.
  3. Na leo ni siku ya kisukari duniani  miaka 100 tangu kugunduliwa kwa ugonjwa huo shirika la afya la Umoja wa Mataifa duniani WHO linasema takriban watu milioni 422 waliishi na kisukari mwaka 2014 na idadi ya wenye ugonjwa huo imeongezeka karibu mara mbili tangu mwaka 1980 kutoka asilimia 4.7 hadi asilimia 8.5. 
  4. Na mashinani ikiwa leo ni Siku ya kutokomeza ugonjwa wa kisukari tutakuletea ujumbe wa WHO kuhusu matumizi ya sukari mbadala na madhara yake.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
10'45"