Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

08 NOVEMBA 2023

08 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anamulika mwelekeo wa El Nino ya kwamba itaendelea hadi Aprili 2024,  halikadhalika madhara  yake, Somalia kulekea uchaguzi mkuu na ushiriki wa wanawake; Makala inabisha hodi Mashariki ya Kati usaidizi wa kibinadamu huko Gaza, na mashinani inabisha hodi Armenia.

  • Tukio la mkondo joto la El Niño linalosababisha hivi sasa mvua kubwa, joto kali na ukame kwenye maeneo mbalimbali ya dunia, linatarajiwa kuendelea duniani na kuchochea ongezeko la kiwango cha joto baharini na ardhini, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Hali ya Hewa, WMO hii leo. Anold Kayanda na maelezo zaidi.
  • Catriona Laing, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia amethibitisha kuwa Umoja wa Mataifa unashirikiana na Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara ya Maendeleo ya Wanawake na Haki za Binadamu nchini humo kuhakikisha kwamba sauti za wanawake zinasikika katika Baraza la Ushauri la Taifa (NCC) ambalo kwa sasa linaundwa na wanaume pekee akiwemo Rais wa shirikisho, marais wa majimbo na viongozi wengine wanaume wa ngazi ya juu ya uongozi.
  • Makala inatupeleka Rafah kwenye mpaka wa Ukanda wa Gaza na Misri ambako Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP kama yalivyo mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu linahaha kuingiza msaada Gaza hususan chakula kwa maelfu ya watu wenye uhitaji Gaza. Mkurugenzi mtendaji wa shirika hilo amefunga safari hadi Rafah kushuhudia hali halisi. Tuungane na Flora Nducha katika makala hii inayoangazia alichoshuhudia.
  • Mashinani fursa ni yake Arevik, ambaye ni mama na mkimbizi wa ndani nchini Armenia, akissema licha ya changamoto walizopitia cha muhimu yuko pamoja na familia yake.
Audio Duration
9'49"