Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

02 NOVEMBA 2023

02 NOVEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, ambapo nchini Tanzania mradi wa Fish4ACP unaofadhiliwa na Muungano wa Ulaya na kutekelezwa na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO kwa kushirikiana n serikali ya Tanzania unaendelea kuleta matunda ya malengo yake ya kuanzishwa. Yaani kuongeza thamani ya mazao yanayotokana na uvuvi na kuimarisha maisha ya wavuvi na wachakataji wa mazao hayo kwa kuongeza thamani. Mradi huu unatekelezwa mikoa ya Kigoma, Katavi na Rukwa. Pi atunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za machafuko Gaza, uhalifu unaofanyiwa waandishi wa habari na ripoti ya UNEP kuhusu Tabianchi na mazingira. Katika kujifunza Kiswahili tunakuletea ufafanuzi wa neno “INADI”.   

  1. Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA imeeleza kuwa mashambulizi za ardhini yanatotekelezwa kwa siku kadhaa sasa na Israel huko katika Ukanda wa Gaza yamezuia usafirishaji wa misaada kutoka Gaza Kusini kwenda Gaza Kaskazini hivyo wananchi walioko Gaza Kaskazini hawawezi kufikishiwa misaada ya kibinadamu wakati huu wakikabiliwa na mashambulizi ya anga na ardhini. 
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira UNEP limezindua ripoti hii leo jijini Nairobi nchini Kenya iliyoeleza maendeleo ya harakati za kuhimili mabadiliko ya tabianchi yanasuasua wakati huu ambapo yanapaswa kushika kasi ili kuendana na ongezeko la madhara ya mabadiliko ya tabianchi. 
  3. Na leo ni siku ya Kimataifa ya kupinga ukwepaji sheria dhidi ya vitendo vya uhalifu wanavyofanyiwa waandishi wa habari ambapo Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amenukuu shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO ambalo linasema mwaka 2022 pekee, waandishi wa habari 88 waliuawa.
  4. Katika kujifunza lugha ya Kiswahili leo ukumbi ni wake mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana ya neno “INADI”.

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'30"