Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

17 JANUARI 2023

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina na tunakupeleka nchini Belize, taifa la ukanda wa karibea kuona jinsi mabadiliko ya tabianchi yamesomba si tu nyumba bali pia makaburi. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kuhusu watoto katika kaya maskini, afya, na hatari zinazokumba wahamiaji. Katika mashinani leo utasikiliza ujumbe kuhusu janga la upatikanaji wa chakula kwa mwaka huu 2023.

Sauti
12'48"

16 JANUARI 2023

Ni Jumatatu tarehe 16 ya mwezi Januari mwaka 2023 na jaridani tunakuletea habari za machungu kutoka DRC pamoja na za kazi ya walinda amani nchini humo. Makala tunakuletea simulizi ya mkimbizi kuhusu safari kutoka Venezuela hadi Chile, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni?

Sauti
11'

13 JANUARI 2023

Jaridani hii leo tutakupeleka Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR na huko Lesvos nchini Ugiriki. Makala tunabisha hodi nchini Rwanda, na mashinani tunakwenda huko Walungu jimboni Kivu Kusini, kulikoni?

Sauti
12'6"

12 JANUARI 2023

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Kenya kumulika harakati za elimu ikiwa ni kuelekea siku ya elimu duniani. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka IAEA, msaada wa kibinadamu nchini DRC na matokeo ya mkutano wa Baraza la Usalama wa Umoja wa Mataifa. Mashinani tunakwenda nchini Uganda. Katika kujifunza kiswahili tunapata ufafanuzi wa msemo "FUNGA FUNGANYA

Sauti
12'2"

11 JANUARI 2023

Jaridan hii leo tutakupeleka nchini Uganda na Somalia. Makala tutamulika uanzishaji wa vikundi vya vijiji vya kukopa na kuweka akiba na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha, na mashinani nchini tunakwenda nchini Ghana, kulikoni?

Sauti
12'35"

10 JANUARI 2023

Jaridani leo tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda Rwanda kumulika harakati za Umoja wa Mataifa na wadau kupunguza vifo vya wajawazito na watoto wachanga. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo haki za binadmu kwa waandamanaji nchini Iran, vifo vya watoto wachanga duniani na virusi vya SARS-Cov-2 vinavyosambaa nchini China. Mashinani tunakwenda nchini Uganda.

Sauti
11'21"

09 JANUARI 2023

Ni Jumatatu ya tarehe 09 ya mwezi Januari mwaka 2023 na katika jarida la habari za umoja wa mataifa tunaangazia changamoto la mafuriko nchini Pakistan na kazi za walinda amani nchini DR Congo.  Makala tutakupeleka nchini Burundi na mashinani nchini Brazil.

Sauti
10'27"
© UNICEF/Asad Zaidi

Mamilioni ya watoto bado wanaishi kwenye maji machafu yaliyotwama nchini Pakistan - UNICEF

Nchini Pakistani, janga la uhai wa mtoto bado ni changamoto kubwa kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko zaidi ya miezi minne iliyopita huku idadi ya maambukizi  ya magonjwa ya hewa na utapiamlo uliokithiri au unyafuzi ikiendelea kuongezeka, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa inajiandaa kwa ajili ya mkutano wa kuchangia taifa hilo la Asia ili lijenge mnepo dhidi ya majanga.

Sauti
2'29"

05 JANUARI 2023

Hii leo jaridani mada kwa kina tukimulika kampeni ya ‘Afya Na Amani’ iliyoanzishwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaotoka Tanzania, TANZBATT 9 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea Habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini Tanzania na DR Congo. Katika kujifunza Kiswahili leo tutaungana na mtaalam wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA kupata ufafanuzi wa msemo "FANYA ILHAM"

Sauti
9'58"