Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

11 JANUARI 2023

11 JANUARI 2023

Pakua

Jaridan hii leo tutakupeleka nchini Uganda na Somalia. Makala tutamulika uanzishaji wa vikundi vya vijiji vya kukopa na kuweka akiba na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha, na mashinani nchini tunakwenda nchini Ghana, kulikoni?

  1. Uganda hii leo imetangaza kutokomeza mlipuko wa ugonjwa wa Ebola uliosababishwa na virusi aina ya Sudan, ikiwa ni chini ya miezi minne tangu kuthibitishwa kwa mgonjwa wa kwanza kwenye wilaya ya Mubende nchini humo 20 mwezi Septemba mwaka jana.
  2. Katika kusaidia jamii hususan za vijijini kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO nchini Somalia linatekeleza mradi wa kisasa wa kuvuna na kuhifadhi maji ili uweza kuwasaidia wakulima na wafugaji katika vijiji vitatu huko Somaliland.
  3. Katika makala ambapo kupitia Mpango wa Pamoja wa Kigoma (KJP), Shirika la Umoja wa Mataifa la maendeleo ya mitaji UNCDF na wadau wake wamewezesha uanzishaji wa vikundi vya vijiji vya kukopa na kuweka akiba na kuimarisha ujuzi wa kidigitali na kifedha wa wanavikundi ili kukabiliana na kikwazo cha kimfumo cha wanavijiji kukosa ujumuishwaji wa kifedha.
  4. Na katika mashinani tunakwenda nchini Ghana kuona jinsi shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF pamoja na wadau wanatekeleza kwa vitendo ujumuishi kwenye michezo. 

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'35"