Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

09 JANUARI 2023

09 JANUARI 2023

Pakua

Ni Jumatatu ya tarehe 09 ya mwezi Januari mwaka 2023 na katika jarida la habari za umoja wa mataifa tunaangazia changamoto la mafuriko nchini Pakistan na kazi za walinda amani nchini DR Congo.  Makala tutakupeleka nchini Burundi na mashinani nchini Brazil.

  1. Nchini Pakistani, janga la uhai wa mtoto bado ni changamoto kubwa kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko zaidi ya miezi minne iliyopita huku idadi ya maambukizi  ya magonjwa ya hewa na utapiamlo uliokithiri au unyafuzi ikiendelea kuongezeka, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto,  UNICEF wakati huu ambapo jumuiya ya kimataifa inajiandaa kwa ajili ya mkutano wa kuchangia taifa hilo la Asia ili lijenge mnepo dhidi ya majanga.
  2. Kikosi cha 9, TANZBATT 9 cha wanajeshi walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC chini ya Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo DRC-MONUSCO, wameendelea na kampeni yao ya Afya na Amani ambapo hadi tarehe 13 mwezi huu wa Januari watakuwa wakiendelea kutoa misaada kwa jamii inayoishi katika eneo lao la kazi, kaskazini mashariki mwa nchi.
  3. Katika makala Edouige Emeresenge, mwandishi wa habari wa Televisheni washirika wetu Mashariki TV, nchini Burundi akimulika harakati za Umoja wa Mataifa kufanikisha lengo namba 3 la malengo ya maendeleo endelevu, SDGs kuhusu elimu bora.
  4. Na katika mashinani tutasikia kauli ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu ghasia zinazoendelea nchini Brazil wakati huu ambapo baadhi ya wananchi wamevamia taasisi ikiwemo bunge. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
10'27"