Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

05 JANUARI 2023

05 JANUARI 2023

Pakua

Hii leo jaridani mada kwa kina tukimulika kampeni ya ‘Afya Na Amani’ iliyoanzishwa na walinda amani wa Umoja wa Mataifa wanaotoka Tanzania, TANZBATT 9 huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC. Pia tunakuletea Habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini Tanzania na DR Congo. Katika kujifunza Kiswahili leo tutaungana na mtaalam wetu Onni Sigalla kutoka BAKITA kupata ufafanuzi wa msemo "FANYA ILHAM"

  1. Siku chache baada ya Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kutangaza kuondoa marufuku ya vyama vya siasa nchini humo kufanya mikutano ya kisiasa, Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa haki za Binadamu imezungumzia hatua hiyo kama asemavyo msemaji wa ofisi hiyo Seif Magango.
  2. Huko nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ujumbe wa Umoja wa MAtaifa wa kulinda amani, MONUSCO umeendelea na jukumu lake la kulinda raia ambapo katika doria ya hivi karibuni zaidi walinda amani kutoka Morocco wameendesha doria katika mji wa Kitchanga jimboni Kivu Kaskazini, eneo ambalo awali ilikuwa vigumu kufikika kutokana na ukosefu wa usalama usababishwao na mashambulizi kutoka kwa waasi.
  3. Na tukitamatishia huko huko DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO limeendelea kusaidia harakati za jamii za kuelimishana kuhusu ugonjwa wa kipindupindu ambao umeripotiwa kukumba wakimbizi wa ndani walio kwenye kambi zilizoko ukanda wa afya wa Nyiragongo jimboni Kivu Kaskazini.
  4. Na katika kujifunza Kiswahili leo mtaalam wetu  Onni Sigalla Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa  nchini Tanzania , anatufafanulia maana ya msemo "FANYA ILHAM". 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu !

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'58"