Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

16 JANUARI 2023

16 JANUARI 2023

Pakua

Ni Jumatatu tarehe 16 ya mwezi Januari mwaka 2023 na jaridani tunakuletea habari za machungu kutoka DRC pamoja na za kazi ya walinda amani nchini humo. Makala tunakuletea simulizi ya mkimbizi kuhusu safari kutoka Venezuela hadi Chile, na mashinani tunakwenda nchini Somalia, kulikoni?

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulio lililotokea jana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa moja huko Kasindi, jimboni Kivu Kaskazini..
  2. Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo  wamekabidhi jengo kwa ajili ya mahali pa wagonjwa na wahudumu wa afya kula chakula katika Kituo cha Afya cha Mavivi, mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.
  3. Na Assumpta Massoi anakuletea makala kuhusu tamu na chungu ya safari ya kutoka Venezuela hadi Chile kusaka maisha bora!
  4. Na katika mashinani tutasikia kuhusu shehena ya msaada uliotolewa na UNICEF nchini Somalia. 

Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu! 

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
11'