Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

UN Photo/Eskinder Debebe

Mazungumzo yanaendelea kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi kabla ya misaada kuingia Gaza

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza. 

Sauti
3'1"