Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 OKTOBA 2023

24 OKTOBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo ni siku ya Umoja wa Mataifa, chombo kilichoanzishwa mwaka 1945 baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia ikiwa na wanachama waanzilishi 51, bara la Afrika likiwa na nchi nne tu ambazo ni Misri, Liberia, Ethiopia na Afrika Kusini enzi hizo ikijulikana kama Muungano wa Afrika Kusini. Kwa mujibu wa Chata iliyoanzisha chombo hicho, lengo ni kuendeleza amani na usalama duniani, kusongesha uhusiano wa kirafiki baina ya nchi, kufanikisha ushirikiano wa kimataifa na kuwa kitovu cha kuratibu vitendo vya mataifa. Dkt. Kaanaeli Kaale, Mhadhiri Msaidizi katika Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino, SAUT nchini Tanzania, na pia Mtaalamu wa Mawasiliano ya Kimataifa anaeleza iwapo malengo ya kuanzishwa bado yana mantiki. Pia tunakuletea habari kwa ufupi, na mashinani ambapo tunasikiliza ujumbe wa Katibu Mkuu kuhusu siku ya UN.

  1. Ni siku ya 17 ya kuendelea mzozo wa karibuni baina ya Israel na kundi la wanamgambo wa Kipalestina la Hamas huko Mashariki ya Kati Masharikika ya Umoja wa Mataifa yameendelea na kilio cha kuongeza misaada zaidi kuingia Gaza kwani iliyowasili hadi sasa haikidhi mahitaji.
  2. Leo ni siku ya Umoja wa Mataifa inaadhimishwa kumbukumbu ya kuanza kutumika kwa chata iliyoanzisha Umoja huo mwaka 1945. Katika ujumbe wake wa siku hii Clementine Nkweta-Salami naibu mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan na kaimu mratibu mkazi na wa masuala ya kibinadamu amesema “Mwaka huu tunaadhimisha siku hii wakati Sudan ikikabiliwa na moja ya mgogoro  wa kibinadamu unaokuwa kwa kasi ukiambatana na mahitaji makubwa. Mapigano yamegeuza mgogoro huo kuwa janga kubwa. Zaidi ya watu milioni 5.6 wamefurushwa makwao, milioni 25 wanahitaji msaada, zaidi ya wanawake na wasichana milioni 4.2 wako katika hatari ya ukajtili wa kijinsia na mtoto 1 kati ya 3 hana fursa ya kwenda shule. 
  3. Na shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema theluthi mbili ya watoto wakimbizi nchini Armenia wameandikiswa katika mifumo ya kitaifa ya shule mwezi mmoja baada ya watoto 21, 000 wenye umri wa kwenda shule kukimbia makwao. UNICEF imesema sasa juhudi ni kuhakikisha watoto walioasalia 1 kati ya 3 ambao hawahudhurii shule wanapata fursa hiyo.
  4. Na katika mashinani tunasalia katika siku ya Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa chombo hicho anazungumzia nafasi ya kila mtu katika kusongesha malengo ya Umoja wa Mataifa.

Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'40"