Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

31 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tuakuletea mada kwa kina na tunakwenda nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kumulika kampeni ya chanjo iliyomalizika jana Jumanne.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo za afya, haki za binadamu na wakimbizi. Katika mashinani tutakupeleka Geneva nchini Uswisi kupata ujumbe wa shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na UKIMWI, UNAIDS kuhusu kizazi cha watato ulimwenguni ambao wako hatarini kusahaulika.      

Sauti
11'26"

30 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tuakuletea habari njema kuhusu afya na pia kuangazia jamii ya Benet nchini Uganda wakiwa bado hawana utaifa. Makala tunakwenda nchini Kenya na mashinani tunasalia huko huko Kenya, kulikoni?

Sauti
12'

27 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tuakuletea ujumbe wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres kuhusu makumbusho ya Holocaust, pia tunamulika kazi ya walinda amani nchini DR Congo. Makala tunakwenda nchini Tanzania na mashinani tunasalia hapa makao makuu wa Umoja wa Mataifa.

Sauti
11'19"

26 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina ambapo leo tunakwenda nchini Kenya kuangazia juhudi za mradi wa Teen Seed Africa unavyorejesha matumaini ya elimu kwa wasichana walioacha shule kutokana na mimba za mapema.  Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikiwemo kutoka nchini DR Congo, Ethiopia na Senegal. Katika kujifunza Kiswahili   ambapo utapata ufafanusi wa msemo "TABIA NI NGOZI."

Sauti
12'15"

25 JANUARI 2023

Hii Leo jaridani tunaangazia mkutano nchini Niger kuhusu kanda ya Ziwa Chad, na habari njema kwa wakulima wa vitunguu nchini Sierra Leone. Makala tunakupeleka nchini Kenya na mashinani nchini Uganda, kulikoni?

Sauti
11'38"

24 JANUARI 2023

Ni Jumanne ya tarehe 24 mwezi Januari mwaka 2023 ambapo leo tunakwenda nchini Tanzania kuangalia juhudi zinavyofanyika kuhakikisha wanafunzi hususan wa vijijini wanakuwa na mazingira bora ya kuweza kujisomea  nyakati zote. Pia tunakuletea habari kwa ufupi zikimulika hali ya usalama DR Congo, ujumbe wa Katibu Mkuu ya siku hii ya elimu duniani na ripoti ya usafirishaji haramu wa binadamu. Katika mashinani tunakupeleka nchini Kenya.

Sauti
13'7"

23 Januari 2023

Hii leo jarida linaangazia afya likikuletewa ripoti kuhusu ugonjwa wa moyo na WHO na, na pia tuanakupeleka nchini Madagascar kuangazia miradi mbalimbali. Makala na mashinani tunakwenda nchini Rwanda, kulikoni?

Sauti
12'33"

20 JANUARI 2023

Hii leo jarida linaangazia mapigano Soledar Mashariki mwa Donetsk Oblast nchini Ukraine, na habari kuhusu afya kanda ya ulaya. Makala tunakwenda nchini Somalia na mashinani DR Congo.

Sauti
12'1"

19 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tuna habari kwa ufupi, mada kwa kina na jifunze lugha ya kiswahili.

Katika Habari kwa Ufupi na Leah Mushi:

  1. Kuelekea siku ya kimataifa ya elimu tarehe 24 Januari, Mkurugenzi Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO Bi. Audrey Azoulay, amesema ametoa heshima ya siku hiyo kuwa maalum kwa wanawake na wasichana wa Afghanistan ambao mamlaka ya Taliban imewanyima fursa ya kupata elimu.

Sauti
11'12"

18 JANUARI 2023

Hii leo jaridani tunakupeleka Davos Uswisi kusikiliza hotuba ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na pia kuangazia tuzo ya mwaka 2023 iitwayo Crystal Award. Makala na mashinani tunasalía huko huko, kulikoni?

Sauti
11'42"