27 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani Leah Mushi anamulika Gaza, siku ya nne ya sitisho la mapigano; kisha kauli ya shirika la Umoja wa Mataifa la afya ulimwenguni, WHO kulekea COP28. Makala ni kauli ya muathirika wa mapigano huko Mashariki mwa DRC na mashinani mnufaika wa kilimo endelevu kutoka Kenya.
24 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama katika ukanda wa Gaza na msaada wa kibinadamu nchini Chad. Makala tunakupeleka nchini Tanzania, na mashinani tunamulika Ibara ya 13 ya Tamko la Haki za Binadamu.
22 NOVEMBA 2023
Hii leo jaridani tunaangazia tunaangazia mizozo katika ukanda wa Gaza na hali ya mateka waliochukuliwa wakati wa shambulizi la Hamas huko Israel Kusini Oktoba 7. Pia tunamulika amani nchini Sudan Kusini. Makala tunakupeleka nchini Tanzania na mashinani Ufalme wa Tonga katika bahari ya Pasifiki, kulikoni?