27 OKTOBA 2023
Pakua
- Hali Mashariki ya Kati inazidi kuwa mbayá. Mkuu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa leo amezisihi pande zote katika mzozo kusitisha uhasana , huku mashirika ya misaada yakionya kuhusu janga kubwa zaidi la kibinadamu, wakati hapa Makao Makuu kikao cha 10 cha dharura kuhusu mzozo huo wa Mashariki ya Kati kikiendelea leo.
- Wakati maelfu ya wananchi wakikimbia machafuko nchini Sudan mashirika ya Umoja wa Mataifa nayo yana haha huku na kule kuhakikisha wanatoa usaidizi kwa wakimbizi hao.
- Katika makala Assumpta Massoi anazungumza na Mutua Muthusi, Mkurugenzi wa Maendeleo ya Ushirikiano kutoka shirika la posta duniani, UPU kuhusu changamoto na fursa za huduma za posta katika nchi zinazoendelea hususan barani Afrika hasa wakati huu wa maendeleo ya kidijitali.
- Na mashinani tunakuletea ujumbe wa Everlyne Lagat kutoka Baringo Kaunti nchini Kenya, mmoja wa wakulima wadogo ambao wameweza kuondokana na hatari ya majanga ya njaa na umasikini kwa kuwa Shirika la Umoja Wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP linanunua chakula cha msaada kutoka kwao
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!
Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'11"