Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 AGOSTI 2023

20 AGOSTI 2023

Pakua

Hii leojaridani tunaangazia ziara ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mashariki ya kati na kilichojiri hapa makao makuu baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huko kugonga mwamba. Makala tunaangazia akili mnemba katika filamu na mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.

  1. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres aliyeko nchini Misri leo ametembelea mpaka wa Rafah, kivuko pekee cha kuingia na kutoka Ukanda wa Gaza, ambako hivi sasa kuna mashambulizi yanaendelea kati ya Israel na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas na kusema hivi sasa wanaendelea na mazungumzo kupata ufafanuzi wa vikwazo na vizuizi vya masharti yaliyowekwa na Israel kabla ya kuruhusu misaada ya kibinadamu kuingia Ukanda wa Gaza.
  2. Mzozo wa Mashariki ya Kati ukiendelea kati ya Israeli na kundi la wanamgambo wa kipalestina, Hamas, hapa makao makuu ya Umoja wa Mataifa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lenye jukumu la kusimamia amani na usalama liko njiapanda baada ya rasimu mbili za maazimio kwa ajili ya kuchukua hatua kwenye mzozo huo kugonga mwamba! 
  3. Makala leo inamulika Akili mnemba ambayo imebadili fani ya sanaa na utamaduni kwa njia ambazo hazikutarajiwa na mabadiliko hayo ni ya muda mrefu. Na kwa kutambua umuhimu wa suala hili shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni, UNESCO limeandaa mjadala maalum kuhusu akili mnemba kwenye sekta ya filamu. Ajenda inajikita kwenye manufaa na changamoto zitakazokumba sekta za utamaduni na sanaa ukizingatia maadili na ubunifu. Yvonne Muinde mchanganya picha za filamu ni msanii aliyebobea kwenye sekta ya ubunifu na dijitali na mshiriki wa mjadala huo wa UNESCO ulioanza jana.
  4. Na katika mashinani tunakupeleka katika ukanda wa Gaza nchini Palestina na utamsikia ujumbe wa mfanyakazi wa Umoja wa Mataifa kuhusu machungu wanayopitia wanawake na wasichana katika eneo hilo.

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
14'33"