Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

22 DESEMBA 2023

22 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC na hali ya usalama katika ukanda wa Gaza.  Makala tuankuletea ujumbe wa mwanariadha Violah Cheptoo kutoka Kenya na mashinani tuankupeleka nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu mazingira na haki za watoto. 

  1. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kazi ya kuhesabu kura inaendelea baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika Jumatano na kuendelea katika baadhi ya maeneo jana Alhamisi, huku ikielezwa kwamba jimboni Ituri, maisha  yamerejea katika hali ya kawaida kwenye eneo la Fataki baada ya mwaka mmoja wa mashambulizi kutoka kwa wanamgambo waliojihami wa kundi la CODECO.
  2. Njaa imeukumba Ukanda wa Gaza kwa mujibu wa shirika la afya la Umoja wa Mataifa WHO na hivyo kutishia ongezeko la magonjwa hususan miongoni mwa watoto, kina mama wajawazito na wanaonyonyesha na makundi mengine yaliyo hatarini na nishati ya kupikia nayo imeota mbawa.
  3. Katika makala Assumpta Massoi anazungumza na mwanariadha wa kimataifa kutoka Kenya wakati alipotembelea hapa Makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York, Marekani mwezi Novemba mwaka huu kwani Umoja wa Mataifa unapigia chepuo michezo kwa afya, ustawi na amani. 
  4. Mashinani tutaelekea nchini Tanzania kusikia ujumbe kuhusu haki za Watoto.   

Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!

Audio Credit
Anold Kayanda
Audio Duration
9'58"