Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

15 DESEMBA 2023

15 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tnaangazia ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania, na wanariadha mashujaa wa mazingira nchini Kenya. Makala tunasalia hapa makao makuu na mashinani tunakupeleka nchini Zimbabwe, kulikoni?.

  1. Baada ya Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la Elimu, Sayansi na Utamaduni, UNESCO kuitambua lugha ya Kiswahili kuwa miongoni mwa lugha za kimataifa, sasa Tanzania imetangaza kwamba kwa kushirikiana na nchi nyingine wataanza kutoa Tuzo za Kimataifa za Kiswahili. Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo wa Tanzania Dkt. Damas Ndumbaro amemweleza hayo mwandishi wa Idhaa hii Leah Mushi aliyehudhuria ufunguzi wa Kongamano la nane la Kimataifa la Chama cha Ukuzaji wa Kiswahili Duniani (CHAUKIDU), uliofanyika leo jijini Arusha kaskazini mwa Tanzania.
  2. Mashirika ya umoja wa Mataifa lile mazingira duniani UNEP na lile la afya WHO nchini Kenya yamehimiza umuhimu wa kuhakikisha mazingira safi kwa ajili ya afya bora katika kampeni maalum iliyofanyika jana Alhamisi walipowaalika wanaridha kadhaa wa Kenya kwenye ofisi za Umoja wa mataifa jijini Nairobi.
  3. Miongoni wa wanariadha hao ni Francis Kipkoech Bowen ambaye kwa takriban miaka 20 amekuwa mkibiaji wa mbio za kawaida na marathon. Amezungumza na Stella Vuzo afisa habari wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa Nairobi UNIS kwanza akishukuru Umoja wa Mataifa kumjumuisha. 
  4. Mashinani tnakuleta ujumbe wa mmoja wa wakimbizi nchini Zimbabwe kuhusu mchango wao katika kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi.  

Mwenyeji wako ni Flora, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'2"