Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

20 DESEMBA 2023

20 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jaridani tunaangazia uchaguzi mkuu nchini DRC, na kampeni ya chanjo ya polio nchini Tanzania. Makala tunamulika DAFI Scholarship Programme nchini Rwanda na mashinani tutaelekea Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa.

  1. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, uchaguzi mkuu wa Rais, Magavana, wabunge na madiwani umefanyika hii leo kama ilivyopangwa licha ya changamoto zilizojitokeza katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Assumpta Massoi amefuatiliana na kutuandalia ripoti hii.
  2. Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linahimiza kila nchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa chini ya miaka 5 wanapatiwa chanjo dhidi ya polio ugonjwa ambao sio tu unasababisha ulemavu kwa watoto lakini pia ukakatili maisha yao.
  3. Katika makala ambayo kwa kuzingatia kuwa leo ni Siku ya Kimataifa ya Mshikamano wa Binadamu, Anold Kayanda anaangazia ‘DAFI Scholarship Programme’ ambao ni Mfuko wa Ufadhili wa Kimasomo kwa ajili ya wakimbizi unaopewa nguvu na Serikali ya Ujerumani kupitia Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). 
  4. Mashinani tunakupeleka Mkoani Kigoma, nchini Tanzania kumsikia kijina mbunifu wa majiko yanayopunguza hewa ukaa.  

Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!

Audio Credit
Flora Nducha
Audio Duration
11'5"