Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

24 Februari 2022

24 Februari 2022

Pakua

Karibu kusikiliza jarida ambapo miongoni mwa utakayo yasikia hii leo ni pamoja na mashirika mbalimbali ya Umoja wa Mataifa yameeleza madhara yanayotokea hususan kwa watoto nchini Ukraine kutokana na mashambulizi. Mathalan shirika la Umoja wa Mastaifa la kuhudumia Watoto UNICEF limesema linatiwa wasiwasi mkubwa kutokana na kuongezeka kwa mashambulizi ambayo yanatoa tishio kubwa kwa maisha na ustawi wa Watoto milioni 7.5 nchini humo.

watoto wenye ulemavu waishio katika kambi ya wakimbizi ya Za'atari nchini Jordan wamejengewa vyoo rafiki kwa hali zao na sasa wanafurahia maisha ikilinganishwa na hapo awali walipokuwa wanatumia vyoo vya jumuiya. 

Kutoka Afrika ya Kati walinda amani wa Tanzania TANBATT-5 wameshiriki katika tamasha la jamii katika kuhimiza elimu. 

na makala ni kutokea nchini Madagacar ambako kumekumbwa na mfululizo wa vimbunga. 

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
12'26"