Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Jarida la Habari

15 Julai 2021

Jaridani Julai 15, 2021 na Assumpta Massoi-

COVID-19 sababisha watoto milioni 23 kukosa chanjo

Makubaliano yafikiwa kuzalisha vipimo vya COVID-19 Brazil na Senegal

Sumu ni tatizo la afya ya umma lakini bado nchi zinapuuza kuweka vituo vya kudhibiti

Sauti
13'2"

14 Julai 2021

Jaridani Jumatano na Assumpta Massoi

Pombe imebainika kuwa kisababishi cha wagonjwa wapya 740,000 wa saratani au kansa kwa mwaka jana wa 2020.

Mafunzo ya kuishi na watoto wenye usonji yaleta manufaa kwa wazazi nchini Argentina.

Maelfu ya wakazi wa Khushal Khan ambayo ni moja ya viunga vya jiji la Kabul nchini Afghanstan wanafurahia hali bora ya hewa na mitaa misafi baada ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ukarabati wa barabara na mitaa  unaosimamiwa na Benki ya Dunia.

Sauti
12'55"

Julai 13, 2021

Hii leo utasikia ripoti ya mashirika ya Umoja wa Mataifa inayoeleza kufunguliwa kwa shule na vyuo vya elimu baada ya kufungwa mwaka jana kutokana na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 kumeacha baadhi ya wanafunzi katika njiapanda kwa sababu kile walichopoteza wakati shule zimefungwa , bado hakuna jitihada za kutosha kuhakikisha wanakipata ili kuepusha kukosa kabisa ufahamu wa kile walichokuwa wamepangiwa kukifahamu. 

Pia utasikia namna mabadiliko yaliyofanywa na WFP ya kutoa fedha kwa wakimbizi yalivyosaidia wakimbizi na wananchi waliowakaribisha. 

Sauti
14'57"

12 Julai 2021

Jaridani hii leo na Assumpta Massoi tutasikia habari kwa ufupi lakini pia tutasikia kuhusu hatua zilizopigwa katika kutimiza malengo ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania hususan lengo namba tatu la upatikanji ya huduma ya afya kwa wote.

Sauti
10'35"

Julai 09, 2021

Katika Jarida hii leo utasikia kuhusu muongo mmoja tangu Sudan kusini ipate uhuru wake, Upigaji kura ili kuruhusu misaada ya kibinadamu iendelee kupitishwa nakupelekwa Syria pamoja na wito wa Katibu Mkuu wa UN Antonio Guterres kwa mawaziri wa Fedha na magavana wa G20 kuhusu usambazaji na uzalishaji wa chanjo ya Corona au COVID-19 

Kwenye mada kwa kina leo tunaangazia madhila wanayokutana nayo wananchi wa Msumbiji

Sauti
10'38"

08 Julai 2021

Jaridani leo Alhamisi Julai 8, 2021

Shirika la Umoja wa Mataifa latoa majokofu ya umeme wa jua kwa ajili ya kuhakikisha wauguzi wanatoa chanjo kwa watoto wachanga.

Pia tunakutana na Maissata Cisse al maaruf Mama Afrika, dereva pekee mwanamke wa malori ya safari ndefu katika ukanda wa Afrika Magharibi.

Idhini ya kuvusha misaada ikikoma Julai 10, Wasyria watakuwa hatarini zaidi - OCHA

Sauti
12'33"

7 Julai 2021

Jaridani leo an Assumpta Massoi-

IFAD yapeleka dola Milioni 882,841 kusaidia wahanga wa COVID-19 Tanzania

Mgao wa fedha kwa kaya maskini waleta mnepo wakati wa COVID-19

na kijana Abel Koka asema jukwaa la Usawa wa Kijinsia la Paris limekidhi matarajio yetu vijana

Sauti
13'7"

Julai 06, 2021

Hii leo Jarida letu linaanza na ofisi ya Kamishna wa Haki za Binadamu kwenye Umoja wa Mataifa, imeelezea wasiwasi kuhusu mlipuko wa ghasia katika siku za karibuni huko Eswatini ghasia ambazo zimeripotiwa kusababisha mauaji au kujeruhiwa kwa makumi kadhaa ya watu waliokuwa wanaandamana kudai demokrasia. 

Pia utasikia kuhusu Hali mbaya ya watoto huko Sudan Kusini pamoja na wakimbizi wa ndani nchini Chad. 

 

Sauti
11'45"

JULY 02, 2021

Karibu usikilize Jarida ambapo leo utasikia kuhusu kurejea kwa operesheni za WFP za kusambaza chakula jimboni Tigray nchini Ethiopia baada ya kusitisha wiki iliyopita kutokana na mashambulizi kutoka jeshi la nchi hiyo. Tayari shirika hilo limepatia msaada wa chakula takriban Watu 10,000 katika eneo la Adi Nebried. WFP inatarajia kuwafikia watu 30,000 mpaka mwishoni mwa wiki hi. 

Katika mada kwa kina hii leo nchini Uganda wakimbizi wanazungumzia hali ya maisha katika janga la COVID-19

Sauti
9'56"

July 01, 2021

Katita Jarida hii leo tunakujuza kuhusu ripoti mpya iliyotolewa leo na Shirika la Mpango wa Maendeleo la Umoja wa Mataifa UNDP inayoonesha usaidizi wa kifedha kwa jamii ili kukabili umaskini uliosababishwa na janga la ugonjwa wa Corona au COVID-19 ulikuwa mkubwa zaidi kwa wananchi wa nchi za kipato cha juu huku wale wa nchi maskini wakiambulia kidogo sana au hata patupu. Pia utasikia kuhusu matumaini ya wakimbizi nchini DRC na Somalia. 

Sauti
12'46"