14 Julai 2021
Pakua
Jaridani Jumatano na Assumpta Massoi
Pombe imebainika kuwa kisababishi cha wagonjwa wapya 740,000 wa saratani au kansa kwa mwaka jana wa 2020.
Mafunzo ya kuishi na watoto wenye usonji yaleta manufaa kwa wazazi nchini Argentina.
Maelfu ya wakazi wa Khushal Khan ambayo ni moja ya viunga vya jiji la Kabul nchini Afghanstan wanafurahia hali bora ya hewa na mitaa misafi baada ya utekelezaji wa mradi mkubwa wa ukarabati wa barabara na mitaa unaosimamiwa na Benki ya Dunia.
Audio Credit
Assumpta Massoi
Audio Duration
12'55"