Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

17 Februari 2020

17 Februari 2020

Pakua

Hii leo jaridani Assumpta Massoi anaanzia nchini Kenya ambako Umoja wa Mataifa umeanza kupatia mafunzo vijana 300 wa jeshi la huduma kwa vijana kwa lengo la kusaidia kudhibiti nzige wa jangwani waliovamia taifa hilo tangu mwezi Desemba mwaka jana. Kisha anakwenda Sudan Kusini ambako walinda amani wa Umoja wa Mataifa wamekarabati na kushehenisha vitabu kwenye maktaba ya watoto mjini Juba. Huko Msumbiji nako mradi wa Umoja wa Mataifa waleta matumaini kwa wavuvi na makala ni nchini Uganda kijana mmoja ajitolea kuhakikisha anatumia ujuzi wa uuguzi kuimarisha afya na mashinani mtoto Tasneem kutoka Syria azungumzia jinsi mashambulizi ya anga yalivyoharibu ndoto yake. Karibu!

Audio Credit
Assumpta Massoi
Sauti
12'20"