Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Guterres: Mzozo wa Mashariki ya Kati sipendelei upande wowote

Guterres: Mzozo wa Mashariki ya Kati sipendelei upande wowote

Pakua

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres hii leo amezungumza na waandishi wa Habari hapa kwenye makao makuu ya Umoja huo muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu wanawake na amani na usalama. 

Asante Assumpta, Katibu Mkuu Guterres amezungumza na waandishi wa habari asubuhi ya leo hapa katika Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani ambapo jambo la kwanza alilosema pindi alipofika mbele ya vyombo vya habari ni kuwa ……. Ameshtushwa na taarifa za upotoshaji za baadhi ya kauli alizozitoa hapo jana Katika mkutano wa Baraza la Usalama uliojadili kuhusu mzozo unaoendelea huko mashariki ya kati. 

Guterres amesema taarifa hizo za upotoshaji zinaonesha kana kwamba alikuwa akihalalisha vitendo vya kigaidi vilivyo fanywa na wanamgambo wa kipalestina wa Hamas.

Guterres amesema “Huu ni uongo, na ilikuwa kinyume chake. “amenukuu taarifa yake akisema…. “Nimelaani bila shaka, vitendo vya kutisha na visivyo na kifani vya Oktoba 7 vya Hamas nchini Israel. Hakuna kinachoweza kuhalalisha mauaji ya makusudi, kujeruhi na kutekwa nyara raia au kurusha roketi kuwalenga raia.”

Katika tarifa  yake ya jana pia amesema alizungumzia malalamiko ya WaPalestina na ananukuu alichosem…. “Lakini malalamiko ya watu wa Palestina hayawezi kuhalalisha mashambulizi ya kutisha ya Hamas na kisha niliendelea na namna nilivyoingilia mgogoro huo nikimaanisha misimamo yangu yote juu ya nyanja zote za mzozo wa Mashariki ya Kati.” 

Guterres amehitimisha taarifa yake hiyo fupi ya dakika moja akisema “Ninaamini nilihitajika kuweka kumbukumbu sawa, hasa kwa heshima ya waathiriwa na familia zao.”

Audio Credit
Leah Mushi
Audio Duration
1'49"
Photo Credit
© WHO