Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

© UNICEF/Safidy Andriananten

WFP na serikali ya Madagascar zaungana mikono kubadilisha jamii za vijijini kusini mwa Madagascar kupitia mradi wa RTT

kupitia mradi wa mabadiliko ya haraka vijijini (RRT) shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa chakula duniani WFP na wadau wake wameanzisha kituo maalum cha paneli za sola ambacho ni chanzo kikuu na endelevu cha maji na teknolojia ya mawasiliano ICT katika maeneo ya vijijini nchini Madagascar, hatua inayoruhusu upatikanaji wa huduma muhimu kama vile nishati, maji na mitandao ya kijamii kwa wakazi wa jamii hizo na kwa njia inayojali mazingira.

Audio Duration
2'35"
Unsplash/Markus Winkler

Mabillioni ya watu ulimwenguni hawajalindwa kutokana na viambato vinavyosababisha ugonjwa wa moyo

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la la Afya Duniani (WHO) iliyotolewa leo Jumatatu Januari 23, 2023 imebainisha kuwa watu bilioni tano duniani hawajalindwa dhidi ya viambato hatari vya mafuta vilivyoko katika bidhaa za vyakula vinazozalishwa viwandani na hivyo kuongeza hatari ya kupata magonjwa ya moyo na kifo.

Sauti
2'55"
Photo courtesy of Ukrainian Women’s Fund

Misaada wawasili kwa mara ya kwanza katika eneo la Donetsk Oblast Ukraine: OCHA

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA limesema kwa mara ya kwanza misaada ya mashirika ya Umoja wa Mataifa imefanikiwa kuwasili katika eno linalodhibitiwa na serikali karibu na Soledar Mashariki mwa Donetsk Oblast nchini Ukraine.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo mjini Geneva Uswis na OCHA msaada huo wa kibinadamu uliosheheni kwenye malori matatu ni kwa ajili ya kuwasaidia zaidi ya watu 800 ambao walisalia katika jamii zinazozunguka eneo la Soledar. 

Sauti
1'43"
WHO-Europe

Kampeni ya utoaji chanjo ya homa ya mafua makali yaendelea ukanda wa ulaya: WHO

Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya ulimwenguni WHO kanda ya ulaya tangu kuanza kwa msimu wa baridi kali katikati ya mwezi Novemba mwaka 2022 wamebaini kuongezeka kwa wagonjwa wanaolazwa kutokana na magonjwa ya homa ya mafua makali au flu,  matatizo ya kupumua na COVID-19. Walio hatarini zaidi kupata maambukizi ya magonjwa hayo ni wahudumu wa afya pamoja na wazee, ndio maana wanaendesha kampeni ya kutoa chanjo. 

Sauti
2'41"
WEF/Pascal Bitz

Guterres atoa onyo kuwa hatuwezi kutatua zahma zinazotukabili katika dunia iliyogawanyika bila mshikamano

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema dunia haiwezi kutatua changamoto kubwa inazokabiliwa nazo hivi sasa kuanzia mabadiliko ya tabianchi, vita ya Ukraine, mdororo wa uchumi na athari zinazoendelea za janga la COVID-19 katikia hali ya sasa ya mgawanyiko na kutokuwa na mshikamano hivyo wakati wa kufumbia macho changamoto hizi umepita na wanaochangia wawajibishwe.

Sauti
2'45"
TANZBATT 9 / Private Sosper Msafiri

TANZBATT 9 nchini DRC wahitimisha kampeni ya Amani na Afya kwa kukabidhi jengo

Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo  wamekabidhi jengo kwa ajili ya mahali pa wagonjwa na wahudumu wa afya kula chakula katika Kituo cha Afya cha Mavivi, mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.

Sauti
3'55"
UN Photo/Mark Garten

Katibu Mkuu UN asisitiza wahusika wawajibishwe kufuatia mlipuko kanisani DRC

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres amelaani vikali shambulio lililotokea jana mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC wakati wa ibada ya Jumapili katika kanisa moja huko Kasindi, jimboni Kivu Kaskazini.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa António Guterres ameanza kwa kutoa pole kwa familia zilizofiwa, watu wa DRC na serikali yao na akawatakia ahueni ya haraka waliojeruhiwa katika shambulio hilo la kilipuzi kilicholipuka katikati ya misa ya jumapili.

Sauti
1'42"
Kapteni Mwijage Francis Inyoma

TANBATT 6 nchini CAR wafanya matibabu kwa wananchi

Wananchi wa eneo la Potopoto nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, wameeleza furaha yao baada ya walinda amani wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MINUSCA kutoka kikosi cha 6 cha Tanzania, TANBAT 6 , kutumia wataalamu wake wa afya kutoa matibabu na dawa kwenye zahanati ya Potopoto wilayani Mambéré-Kadéï.

Kapteni Nashiru Bakari Mzengo Mganga Mkuu wa TANBAT 6 amekabidhi dawa kwa mganga mkuu wa Zahanati ya Potopoto katika wilaya ya Mambéré-Kadéï hapa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Sauti
2'32"