Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

TANZBATT 9 nchini DRC wahitimisha kampeni ya Amani na Afya kwa kukabidhi jengo

TANZBATT 9 nchini DRC wahitimisha kampeni ya Amani na Afya kwa kukabidhi jengo

Pakua

Kikosi cha 9 cha walinda amani wa Umoja wa Mataifa kutoka Tanzania wanaohudumu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kupitia Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo - MONUSCO wamehitimisha kampeni yao ya Afya na Amani iliyoanza tarehe 3 mwezi huu wa January ambapo  wamekabidhi jengo kwa ajili ya mahali pa wagonjwa na wahudumu wa afya kula chakula katika Kituo cha Afya cha Mavivi, mjini Beni, Jimboni Kivu Kaskazini mashariki mwa DRC.

Akikabidhi jengo hilo Kamanda wa kikosi cha tisa cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania Luteni Kanali Barakael Mley amesema jengo hilo litabaki kuwa kumbukumbu ya uhusiano mzuri baina ya walinda Amani wa kikundi cha Tisa na wananchi wa maeneo ya Mavivi na maeneo jirani,

Akiongea kwa niaba ya Maganga mkuu wa hospital ya Oicha na wananchi wa maeneo ya Mavivi Dr Kasereka Nzala amewapongeza walinda Amani hao wa Tanzania wanaohudumu chini ya mwamvuli wa MONUSCO wamekuwa wakifanya jitihada mbalimbali katika kutatua changamoto za wananchi katika maeneo yao ya uwajibikaji,

Kwa upande wake afisa Mahusiano wa kikosi cha tisa cha Ulinzi wa Amani kutoka Tanzania Kepteni Paul Mwesongo amebainisha kuwa hali ya uhusiano baina ya wananchi na walinda Amani hao,

Naye bi Kavathama Clarice, mwenyekiti wa kamati ya Afya katika kituo cha afya cha Mavivi amesema,

Audio Credit
Kapteni Lihaya
Audio Duration
3'55"
Photo Credit
TANZBATT 9 / Private Sosper Msafiri