Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

27 DESEMBA 2023

27 DESEMBA 2023

Pakua

Hii leo jarida linajikita barani Afrika likianzia Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC kuangazia uchaguzi, wapiganaji wa zamani na MONUSCO, halikdhalika Jiko Point na mashinani ni nchini Kenya.

  1. Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, kazi ya kuhesabu kura za Rais kufuatia uchaguzi mkuu uliofanyika tarehe 20 na kuendelea katika maeneo mengine siku zilizofuata, inaendelea huku nao wanufaka wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo, MONUSCO ambao umeanza kufunga virago, wakitoa shukrani zao. Ufafanuzi zaidi anakupataia Anold Kayanda.
  2. Mjini Beni jimboni Kivu Kaskazini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC takribani watu 500 wamenufaika na matibabu ya bure yanayotolewa na walinda aman iwa Umoja wa Mataifa kutoka India, wanaohudumu kwenye ujumbe wa umoja huo wa kulinda amani nchini humo MONUSCO. Evarist Mapesa anafafanua zaidi.
  3. Makala: Leo inatupeleka Tanzania kuzungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya habari na teknolojia ya Nukta Afrika Nuzulack Dausen  ambaye pia mwanzilishi wa Jiko point inayojihusisha zaidi na utoaji habari sahihi kuhusu uhakika wa chakula na lishe, jambo ambalo linapigiwa upatu kila uchao na Umoja wa Mataifa. Amezungumza hivi karibuni jijini Dar es Salaam na Stella Vuzo afisa habari wa Umoja wa Mataifa kufahamu kwa undani wanachokifanya katika kutimiza azma hiyo na anaanza kwa kueleza Jiko point ni nini hasa?
  4. Mashinani: Tutaelekea katika Kaunti ya Turkana nchini Kenya, kumsikia mvuvi ambaye ameweza kuongeza kipato chake na kupunguza upotevu wa chakula kwa msaada wa Umoja wa Mataifa 
Audio Credit
ASSUMPTA MASSOI
Audio Duration
9'57"