Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Habari kwa Ujumla

UNICEF/Henry Bongyereirwe

Lazima tutokomeze ukeketaji : Mwanaharakati Ifra Ahmed

Kutana na mkimbizi kutoka Somalia, muathirika wa ukeketaji ambaye hakuacha athari za jinamizi hilo kusambaratisha ndoto zake za kuhakikisha hatopumzika hadi pale mangariba wote watakapobwaga manyanga na kuacha ukatili huo nchini Somalia na kwingineko duniani. Kulikoni Flora Nducha anasimulia zaidi 

(TAARIFA YA FLORA NDUCHA) 
  Jina langu ni Ifrah Ahmed

Dublin nchini Ireland maskani  ya kudumu ya Ifra mkimbizi wa zamani aliyegeuka kuwa mwanaharakati wa kupinga ukeketaji na sasa anajivunia kuwa raia wa taifa hilo la barani Ulaya. 

Sauti
2'49"
OCHA/Gemma Connell

Corona yachangia ongezeko la ajira za utotoni

Kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miongo miwili, ajira za utotoni zimeongezeka na kufikia watoto milioni 160 na huenda takwimu hizo zikapanda kwa mwaka ujao wa 2022 iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa kuwalinda watoto.

Taarifa hii ipo kwenye ripoti iliyotolewa leo na Mashirika mawili ya umoja wa mataifa lile la kushughulikia watoto UNICEF na la ajira ILO mjini Geneva Uswisi.  Tuungane na Jason Nyakundi kwa ufafanuzi zaidi. 

Sauti
2'18"
© UNICEF/Noorani

Anayepata mimba ya utotoni, asiposoma, kuna uwezekano mkubwa mtoto wake hatosoma

Umoja wa Mataifa kupitia malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, unahamasisha kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, usawa wa kijinsia na mengine kama hayo ambayo kwa pamoja yanamhakikishia mwanadamu ustawi bora wa maisha yake. Nchini Tanzania, wadau mbalimbali wa elimu na masuala ya watoto hususani wa kike, wamekuwa wakipaza sauti za kutaka kubadilishwa kwa sera zinazowazuia watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, kuzuiliwa kuendelea na masomo yao.

Sauti
3'45"
Lin Qi

Asante IFAD! Tumelinda mazingira na kujikinga na COVID-19- Wananchi Ethiopia

Mfuko wa kimataifa wa maendeleo ya kilimo -IFAD umewawezesha wanakijiji nchini Ethiopia kujipatia kipato kupitia mradi wa uchimbaji wa mifereji ya kuzuia maji yasiharibu mazingira na kudhibiti mmonyomoko wa udongo uliokuwa ukiathiri kilimo na hivyo kuwakosesha mapato. Mradi huo pia umewawezesha kujinusuru na maambukizi ya corona.  Jason Nyakundi na maelezo zaidi.

Sauti
2'23"
GEF

Clement abadilika kutoka 'nyoka wa machimbo' hadi mwanafunzi darasani

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limechukua hatua kuwaondoa watoto wachimbaji madini kwenye eneo la Kipushi, jimboni Katanga-Juu na kuwapeleka shuleni, hatua ambayo imeleta furaha kwa watoto hao. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. 

Watoto wakipasua miamba kwa mikono kusaka madini! Mwanamke naye anaponda mawe kujaribu bahati yake! Ni taswira kutoka video ya UNICEF katika eneo la Kipushi jimboni Katanga Juu nchini DRC!  

Sauti
2'
© Japan for UNHCR/Atsushi Shibu

Wakimbizi wanamichezo kuonesha stadi zao huko Tokyo Japan

Kamati ya kimataifa ya Olimpiki IOC imetangaza ushiriki wa timu ya wakimbizi 29 katika mashindando ya Olimpiki yatakayofanyika Tokyo Japan mwezi ujao. Flora Nducha na maelezo zaidi.

Kamishna Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Filippo Grandi akiipongeza timu hiyo ya wakimbizi na kusema anachotarajia kutoka kwao mwezi Julai ni ushindi.  

Sauti
2'32"
IOM/Mashrif Abdullah Al

Taka za plastiki Cox's Bazar zageuka lulu

Udhibiti wa taka ngumu ikiwemo za plastiki ni changamoto kubwa katika kambi ya wakimbizi wa Rohingya ya Cox’s Bazar nchini Bangladesh, na hasa kwa kuzingatia kwamba kambi hiyo ina msongamano na hakuna shemu maalum ya kutupa limesema shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM ambalo  sasa limepata dawa mujarabu. Je ni ipi hiyo? Ungana na Flora Nducha  katika taarifa ifuatayo.

Sauti
2'16"
UN /Manuel Elias

Tanzania yawa Makamu wa Rais UNGA76 na mjumbe wa ECOSOC

Tanzania imechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa mkutano wa 76 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, UNGA utakaoanza tarehe mosi mwezi Septemba mwaka huu. 

Kwa mujibu wa Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Balozi Profesa Kennedy Gastorn, uchaguzi huo umefanywa na nchi wanachama, siku ya Jumatatu Mei 7, Tanzania ikiwa ni miongoni mwa makamu marais 9 wa mkutano huo utakaoongozwa na Rais wa mkutano huo wa 76 Abdulla Shahidi kutoka Maldives. 

Uchaguzi huo pia ulifanyika kumchagua Bwana Shahidi ambaye alimshinda mpinzani wake kutoka Afghanistan. 

Sauti
1'38"
Photo: Sean Kimmons/IRIN

Maambukizi ya VVU Tanzania yamepungua kwa kiasi kikubwa - Rais Samia

Tanzania imesema inaunga mkono mshikamano wa kimataifa wa kutokomeza Ukimwi duniani, kauli iliyotolewa leo na Rais wa taifa hilo Samia Suluhu Hassan wakati akihutubia mkutano wa ngazi ya juu wa Baraza Kuu la  Umoja wa Mataifa kuhusu UKIMWI ulioanza leo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwa njia ya mtandao na ukumbini. Assumpta Massoi na taarifa zaidi.

Mkutano huo wa siku tatu unatathmini maendeleo yaliyofikiwa duniani katika kupunguza maambukizi ya ugonjwa huo tangu kufanyika kwa mkutano wa ngazi hiyo mwaka 2016. 

Sauti
2'6"
TANZBATT_7/ Issa Mayambua

UNHCR yatoa mafunzo ya kutengeneza taulo za kike

Wanawake na wasichana wakimbizi waliotawanywa na machafuko nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC, wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu kupata taulo za kike kila mwezi kutokana na gharama huku wakijaribu kulinda uhai wao, na kuhudumia familia zao baada ya kukimbia vita. Lakini sasa kwa msaada wa mradi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR wanaweza kujishonea taulo hizo na kujisitiri. Flora Nducha anasimulia zaidi