Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Anayepata mimba ya utotoni, asiposoma, kuna uwezekano mkubwa mtoto wake hatosoma

Anayepata mimba ya utotoni, asiposoma, kuna uwezekano mkubwa mtoto wake hatosoma

Pakua

Umoja wa Mataifa kupitia malengo 17 ya maendeleo endelevu, SDGs, unahamasisha kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu, afya, usawa wa kijinsia na mengine kama hayo ambayo kwa pamoja yanamhakikishia mwanadamu ustawi bora wa maisha yake. Nchini Tanzania, wadau mbalimbali wa elimu na masuala ya watoto hususani wa kike, wamekuwa wakipaza sauti za kutaka kubadilishwa kwa sera zinazowazuia watoto wa kike wanaopata ujauzito wakiwa shuleni, kuzuiliwa kuendelea na masomo yao. John Kabambala wa redio washirika KidsTime FM ya Morogoro Tanzania ameliangazia suala hilo ambalo linaanza kupata nuru kutokana na kauli ya waziri wa elimu wa nchi hiyo.

Audio Credit
Assumpta massoi/John kabambala
Audio Duration
3'45"
Photo Credit
© UNICEF/Noorani