Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Clement abadilika kutoka 'nyoka wa machimbo' hadi mwanafunzi darasani

Clement abadilika kutoka 'nyoka wa machimbo' hadi mwanafunzi darasani

Pakua

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto limechukua hatua kuwaondoa watoto wachimbaji madini kwenye eneo la Kipushi, jimboni Katanga-Juu na kuwapeleka shuleni, hatua ambayo imeleta furaha kwa watoto hao. Assumpta Massoi na maelezo zaidi. 

Watoto wakipasua miamba kwa mikono kusaka madini! Mwanamke naye anaponda mawe kujaribu bahati yake! Ni taswira kutoka video ya UNICEF katika eneo la Kipushi jimboni Katanga Juu nchini DRC!  

Umaskini umefikisha watoto na wanawake eneo hili. Clement Kapanda mtoto mwenye umri wa miaka 12 ni manusura wa hali hii na mwokozi wake ni UNICEF. 

Clement anasema alikuwa anatumikishwa kwenye uchimbaji madini na wakati mwingine hakuwa na chakula. 

Clement walitumbukia kwenye mashimo marefu wakitumia vyuma kupasua miamba!  

Wengine walitumia vifaa duni kupasua mawe yaliyokwishachimbwa na hata kuharibu mikono na miguu yao.  Video hiyo inaonesha mchakato mzima wa uchimbaji madini kuwa hatarini na hatma yake ni malori kufika eneo hili na kubeba vifusi kupeleka vitakiwapo.  

UNICEF sasa imemuondoa Clement machimboni na kumweka darasani na anaonekana akisikiliza kwa makini.  Clement ana furaha na wahudumu wa kijamii wanapita sasa mitaani kuwasihi wazazi wapeleke watoto wao shuleni ili wapate haki yao ya msingi ya kuendelezwa. 

Audio Credit
Leah Mushi/Assumpta Massoi
Audio Duration
2'
Photo Credit
GEF