Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sasa kutakuwa na amani kati ya wakazi wa Boeing na PK5 mjini Bangui, CAR

Sasa kutakuwa na amani kati ya wakazi wa Boeing na PK5 mjini Bangui, CAR

Pakua

Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, MINUSCA umejenga kituo cha mafunzo kwa ajili ya vijana wasio na ajira kwenye mji mkuu wa nchi hiyo Bangui, ikiwa ni sehemu ya miradi yake ya matokeo ya haraka, QIPS.  Assumpta Massoi na maelezo zaidi.

Kituo hicho kinalenga vijana wa kata za Boeing na PK5 ambapo wamepatiwa vifaa katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa Bimbo mjini Bangui, mradi ukilenga kuimarisha amani kupitia kuwapatia vijana ajira zenye utu. 

Joel Presley Donasse ambaye ni Katibu Mkuu wa ukumbi wa Bimbo amesema, “tuko katika mwelekeo wa kuona faida, tunaanza tuko katika mwelekeo wa kushuhudia kitu. Tuna furaha sana kwa mabadiliko ambayo yatatokea katika jamii yetu.” 

Vifaa hivyo in pamoja na mashine tatu za kushonea nguo, jozi moja ya paneli za sola, betri kubwa moja, feni na viti. 

MINUSCA inasema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa vitasaidia sana kuimarisha amani na pia uhusiano kati ya jamii za Boeing na PK5 na pia kuongeza ujuzi wao. 

Gilles Guigui ni afisa wa masuala ya kiraia MINUSCA na anasema “MINUSCA inaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya CAR kupitia miradi yake ya matokeo ya haraka. Katika kipindi cha mwaka 2019/2020 tuko kwenye harakati za kutekeleza makumi kadhaa ya miradi ya matokeo ya haraka kwenye mji wa Bangui na viunga vyake, kwa ushirika na mashirika ya kiraia ya hapa nchini na ya kimataifa.” 

Audio Credit
Anold Kayanda/Assumpta Massoi
Audio Duration
1'39"
Photo Credit
MINUSCA/Hervé Serefio