UNESCO yaonya kuwa bila hatua za haraka watoto milioni 12 hawatowahi kutia mguu shuleni
Takwimu mpya zilizochapishwa leo na kitengo cha takwimu cha shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCOkuhusu Watoto wasiohudhuria shule zinaonyesha kwamba hakuna hatua yoyote iliyopigwa au kuna hatua ndogo sana ilipyopigwa kwa zaidi ya muongo mmoja.